……………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt. Pindi ametoa wito kwa jamii kupanda miti kwa kuwa upo uhitaji mkubwa wa bidhaa zinazotokana na misitu ndani na nje ya Tanzania.
Aidha, ameeleza kuwa miti ni fursa muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja naTaifa kwa aujumla.
Balozi Dkt. Chana ameyasema hayo alipotembelea Shamba la Miti la Sao Hill, Kiwanda cha Lush Chanzo kinachotengeneza bidhaa mbadala ya mbao (MDF), pamoja na Mradi wa Maendeleo Endelevu ya Misitu (FDT), wilayani Mafinga mkoa wa Iringa.
Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana licha ya kuwapongeza wadau wa Maliasili na Utalii kwa uwekezaji mkubwa kwenye misitu na uchakataji wa Mazao ya Misitu, amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ili kuiendeleza sekta hiyo hapa nchini.
Akielezea hatua mbalimbali za uhifadhi wa Misitu Mhifadhi Mkuu wa Shamba Miti la Sao Hill Lucas Sabida amesema licha ya kuwa na Shamba kubwa la miti waneendelea kuotesha miche zaidi ya miti, kuelimisha na kuishirikisha jamii katika kuhakikisha inaongeza umiliki wa mashamba ya Miti.