………………………………
Makamu wa Rais wa Uganda Mhe Jessica Alupo ametembelea Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea na Urithi adhimu na adimu wa Historia ya Tanzania uliohifadhiwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Mhe Alupo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, na kupatiwa maelezo ya Uhifadhi wa Uridhi wa Utamaduni na Historia kutoka kwa Wataalam wa Makumbusho hiyo.
Alikuja nchini kwa kuudhuria Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara chini ya Mkataba wa Eneo huru la biashara Afrika uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Jijini Dar es Salaam.
Mhe Alupo aliipongeza Makumbusho ya Taifa kwa uhifadhi unaofanyika na kuahidi kurudi tena
“Nimefurahishwa sana na uhifadhi unaofanyika hapa, Makumbusho hii ipo vizuri maoneaho na mpangilio wake uko vizuri, hongereni sana’ alisema Mhe Alupo.
Makamu wa Rais huyo alitembelea Onesho la Mchango wa Tanzania katika Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika chini ya uongozi wa baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere ambalo pia linaonesha mchango wa wanawake katika mapambano dhini ya ukoloni.
Vile vile alitembelea ukumbi wa maonesho wa Chimbuko la Mwanadamu na chumba maalum kinachohifadhi tunu za Taifa ikiwa ni pamoja na fuvu halisi la zanadamu
Aidha, alimshukuru mkurugenzi wa makumbusho ya taifa la Tanzania kwa mapokezi mazuri alioyapata kutoka kwa wahifadhi wote kuanzia anaingia hadi anaondoka na kuahidi kwa kusema kuwa:
“Nikipata nafasi nitarudi tena kutembelea na kujifunza vizuri historia kwa sababu inatusaidia kuendeleza vizazi vya sasa na vijavyo kujua historia yetu, ‘ Makamu wa Rais nchini Uganda.