………………………………
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Sekta za Maliasili na Mazingira wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Bw. Nathan pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Ujerumani nchini (GIZ), Dkt. Falconk.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa nyakati tofauti Septemba 13, 2022 jijini Dodoma, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Maliasili na Utalii. Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha