Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Meja Jenerali Hamisi Semfuko akizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari katika pori la akiba la Pande walipotembelea katika pori hilo ili kuona shughuli mbalimbali za uhifadhi zinazofanywa na TAWA kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Jane Mihanji, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TAWA Mabula Misungwi Nyanda na kulia ni  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Meja Jenerali Hamisi Semfuko akimsikiliza Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TAWA Mabula Misungwi Nyanda wakati akizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari katika pori la akiba la Pande walipotembelea katika pori hilo ili kuona shughuli mbalimbali za uhifadhi zinazofanywa na TAWA kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Jane Mihanji  na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile akizungumza katika kikao hicho.

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Neville Meena akifafanua jambo katika kikao hicho.

Picha ya pamoja

Baadhi ya wahifadhi wakiwa katika kikao hicho.

Picha zikionesha wahariri mbalimbali wakifuatilia uwasilishaji wa mada katika kikao hicho.

Mhifadhi Noti Mgaya akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Meja Jenerali Hamisi Semfuko, Viongozi na wahifadhi mbalimbali wa TAWA pamoja na wahariri wa vyombo vya habari wakati walipotembelea pori la akiba la Pande Mabwepande jijini Dar es Salaam

Vick Kamata Mkuu wa KItengo cha Uhusiano Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania TAWA akiwakaribisha wahariri kutoka vyombo mbalimbali katika pori la akiba la Pande Mabwepande wakati walipotembelea pori hilo ili kujifunza na kupata uelewa wa shughulimbalimbali za Mamlaka hiyo katika uhifadhi.

……………………………………………

Imeelezwa kuwa uvamizi wa Mifugo Katika maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba umeendelea kupungua kila Mwaka kutokana na doria inayoimarishwa na Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania-TAWA Kwenye maeneo hayo.
Hayo yameelezwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TAWA Mabula Misungwi Nyanda wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Pamoja na waaandishi wa habari katika pori la akiba la Pande Mabwepande jijini Dar es salaam.
Nyanda amesema kuwa kati ya Mwaka wa 2016/2017 na 2020/2021 Mifugo iliyokamatwa katika mapori ya Akiba ilipungua kwa Asilimia 65.5 Kutoka Mifugo 58,708 Mwaka 2016/17 Hadi Mifugo 19554 kufikia Mwaka 2021.
Aidha amesema malengo Mkakati yao ni kuhakikisha wanaimarisha Ulinzi wa rasilimali wanyamapori pamoja na Malikale,kuboresha huduma za utalii  lakini pia kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa mamlaka hiyo.
“Katika kuimarisha Ulinzi tumejitahidi kupunguza kasi ya ujangili na hivyo kufanya matukio ya mauaji ya tembo kupungua kutoka tembo 18 kwa Mwaka 2016/ 2017 na mpaka watatu Mwaka 2020/2021 na pia katika mapori ya Akiba Selou imepungua”amesema Nyanda
Vilevile amesema wamekuwa wakiwashirikisha wananchi katika kunufaika na uhifadhi ambapo Mamlaka iliandaa muongozo wa kusimamia shughuli za uvuvi na ufugaji nyuki katika maeneo hayo.