Shabiki wa klabu ya Simba wa mkoa wa Arusha, Joseph Marwa akipozi na mfano wa hundi baada ya kushinda Sh60, 321,350 kupitia mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet. Marwa ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.
…………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Shabiki wa klabu ya Simba anayeishi mkoani Arusha, Joseph Marwa ameshinda sh60, 321,350 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.
Marwa ambaye ni mjasiriamali alisema kuwa awali hakuwa na imani na michezo ya kubashiri kabisa mpaka alipofuatwa kukopwa fedha ya nauli na mmoja wa washindi kampuni ya M-bet.
Alisema kuwa mshindi huyo alimfuata kumkopa nauli ya kwenda Dar es Salaam na kuahidi angemrudishiwa mara baada ya kupokea fedha alizoshinda.
Alifafanua kuwa kwa vile alikuwa pamoja na kumfahamu mshindi, bado alikuwa anasita kumkopesha kwani kipindi hicho hakuwa na Imani na michezo ya kubashiri.
“Nilimpa Sh150,000 mshindi na rafiki yale ambao walikuja Dar es Salaam kufuata fedha hizo. Sikuwafuatilia kabisa sababu walikuwa vijana ninao wafahamu, lakini mara baada ya kurejea, kijiana alinirejeshea fedha yangu na kwa kuongeza Sh50,000 zaidi.
Sikuamini kabisa na kuanza kumhoji maswali kadhaa na baadaye kumuomba anifundishe kuweka mkeka. Alifanya hivyo na siku ya kwanza tu tokea kuanza kubashiri, nilishinda 800,000 na zaidi ambazo nilitumiwa kwenye simu.
Tokea hapo nikaanza kubashiri na M-bet na kushinda fedha mbalimbali kabla ya kuibuka mshindi katika Jackpot,” alisema Marwa.
Marwa pia aliwapa rai vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kuacha kutumia sh1,000 kununua sigara na kuvuta wakati wanaweza kutumia fedha hiyo kubashiri na M-bet na kujishindia mamilioni ya fedha kama yeye.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-bet, Allen Mushi alisema kuwa Marwa anakuwa mmoja wa wanachama wa nyumba yao ya mabingwa kwani ni mshindi wa tisa wa Jackpo tokea kuanza mwaka huu.
“Tunaposema M-bet ni nyumba ya mabingwa tunakuwa na maana maalum, mpaka sasa tumewazadia mamilioni washindi nane na wameweza kubadili maisha yao.” Alisema Mushi.