Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi maalum Dkt . Doroth Gwajima akizungumza katika mkutano wa siku mbili uliuowakutanisha wadau wa huduma za Ustawi wa Jamii nchini kwenye ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es Salaam leo Septemba 6,2022.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi maalum Dkt . Doroth Gwajima akizindua mwongozo wa malezi ya watoto na Katibu Mkuu wa Wizara wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi maalum Dk. Zainab Chaula na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza katika mkutano huo wa wadau.
Wadau mbalimbali wakiwa wameshikilia muongozo huo mara baada ya kuzinduliwa.
Picha ya pamoja.
…………………………………….
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi maalum Dkt . Doroth Gwajima ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi na walezi wote watakaobainika kuwaachia watoto kuondoka nyumbani na kuingia mitaani na kufanya shughuli mbalimbali .
Waziri Dkt Doroth Gwajima ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku mbili uliuowakutanisha wadau wa huduma za Ustawi wa Jamii nchini.
Katika mkutano huo Dkt. Gwajima amesema serikali ya awamu ya Sita kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuungana na wadau wote wa ustawi wa jamii wanakuja na mpango maalum utakaofanikisha kuondoa mtandao mzima unaofanikisha kuzagaa kwa watoto mitaani katika miji mbali mbali hapa nchini .
Aidha waziri huyo pia amesema wizara yake imeona kuna umuhimu wa kutungwa kwa sheria maalum itakayo komesha vitendo vya baadhi ya watu wenye ulemavu wanaotuimia viti vyenye magurudumu kutumia ulemavu wao kwa kuomba omba kitendo alichosema kinaongeza kundi la Ombaomba mitaani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza katika mkutano huo amesema kwa kushirikiana na wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum tayari wanampango kazi la kuwajengea mazingira mazuri ya kuwatambua watoto wa mitaani na omba omba kwa kuangalia mahala watakapopelekwa mara baada ya kuondolewa mitaani.
Mkutano huo wa wadau wa huduma za Ustawi wa Jamii umekwenda sambamba na uzinduzi wa vitabu viwili ikiwemo kitabu cha Kanuni za Maadili ya kufanya kazi na watoto pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kiongozi cha penzi kitakachosaidia kutoa muongozo katika vituo vya kulelea watoto mchana .