Meneja wa NMB Jogging Club Bi.Stella Motto akizungumza na waandishi wa habari wakati wakati mazoezi ya Jogging yaliyowahusisha NMB na ETV pamoja na EFM ikiwa ni maandalizi ya NMB Marathon.
Mwakilishi wa Vituo vya TV E na EFM ambaye pia ni mtangazaji Bi.Tunu Hassan akifafanua jambo Kwa waandishi wa habari alipozungumza nao kuhusu maandalizi ya NMB Marathon.
Benki ya NMB kwa kushirikiana na vituo vya TV E na EFM wameandaa mbio za NMB Marathon zitakazofanyika Septemba 24, 2022 jijini Dar es Salaam ili kusaidia wakina mama wenye matatizo ya Fistula fedha ambazo zitapatikana kwenye mbio hizo zitakwenda moja kwa moja kwenye matibabu katika hospitali ya CCBRT.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 5,2022 Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Vituo vya TV E na EFM Bi.Tunu Hassan mesema mwanajamii ambaye anaweza kushiriki mbio hizo au kama hataki kushiriki kwa maana ya kukimbia anaweza akashiriki katika kusaidia jamii hasa akinamama ambao wanapitia matatizo hayo.
“Unapochangia elfu 20 yako ama elfu 30 unakuwa umesaidia kwa uwanda mpana sana, wakina mama wakipata matibabu linakuwa jambo zuri kwahiyo tunawaomba watu ambao wanapenda michezo ama mdau yeyote kujitoa ili kusaidia wakinamama hao kupata matibabu”. Amesema
Naye Meneja wa NMB Jogging Club Bi.Stella Motto amesema katika mbio hizo lengo ni kukusanya kiasi cha shilingi Milioni 600 ambazo zitakwenda kusaidia wakinamama wenye matatizo ya Fistula.
Amewaomba wadau mbalimbali wakubwa na wadogo kujitokeza ili kuungana kwa pamoja na NMB kufikisha lengo matibabu ya Fistula.