Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Namanga Tegeta Dar es salaam limeandaa sherehe ya kumletea Matunda Chanzo Halisi ya Shamba lake.
Akizungumza jana na Waandishi wa habari kanisani hapo, Baba Halisi wa kanisa hilo amesema kuwa sherehe hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa kanisa hilo jumapili ya Agost 28 mwaka 2022.
“Sherehe hizi zitafanyika kuanzia saa moja asubuhi hadi saa sita mchana hapa kanisani,dhumuni la kanisa Halisi la Mungu baba kuandaa sherehe hiyo ni kumshukuru Mungu kwa zawadi ya kuilinda Tanzania na majanga mbalimbali, ambapo sherehe hiyo inaenda kufanyika ikiwa ni kusheherekea kile kinachoitwa Matunda ya shamba lake ( Mathayo 21:43) amesema Baba Halisi.
Nakuongeza kuwa “tumepona janga la Kimbunga Job,tumepona milipuko ya magonjwa kama vile Corona, tumepona njaa, tumepona mgao wa umeme,tumepona ukame,tumepona jangwa,tumepona maandamano ya vurugu mitaani ,tumepona volcano , Taifa tumevuka na kadhalika,kwa haya machache na mengine ni vema wote bila kujali kusanyiko la Dini au dhehebu lolote tuje kusherehekea pamoja” amesema.
Aidha kupitia taarifa aliyoitoa kwa waandishi wa habari Baba halisi ametumia maandiko matakatifu akisema kuwa”kitabu cha Kumbukumbu 28:47-48; kinasema kuwa kwakuwa hukumtumikia Bwana Mungu wako ,kwa furaha na moyo wa kushukuru kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote ( 48) kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako , kwa njaa na kwa kiu,na kwa uchi kwa unitaji wa vitu vyote, naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako hata atakapokwisha kukuangamiza”
Nakuongeza kwamba “Efeso 4:6 ‘ kinasema kwamba kuna Mungu mmoja na baba wa wote , ambaye yuko juu ya wote ,anafanya kazi katika yote na yuko katika yote”.
Aidha Baba Halisi amesema kuwa sherehe hiyo inafanyika kanisani hapo huku akiwaalika waumini wa madhehebu na dini zote ndani na nje ya nchi ya Tanzania