Afisa Mtendaji Mkuu Chuo Cha Taifa Cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka akiongea na wanahabari leo jijini Dar kuhusu uzinduzi wa mafunzo kwa wadau wa myororo wa utalii nchini wenye lengo la kuboresha huduma bora kwa mteja (best customer care).
Mafunzo hayo yanazinduliwa kesho na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana kwa kuhusisha maafisa Uhamiaji 700.
CEO Sedoyeka tayari wanahabari wamempachika jina la “Mama wa Pasi” baada ya kutaja malengo ya mafunzo hayo kuwa kama mbinu chanya za kucheza na pasi (fursa) nyingi za Mama (Mhe. Rais) Samia alizotoa kwa wadau wa sekta ya Utalii, baada ya kuupiga mwingi katika Royal Tour.