NA KHALFAN SAID, BUMBULI
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako ametembelea kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Bumbuli,
Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na kuwahakikishia wakulima wa zao hilo kwamba
kiwanda kimekamilika kwa asilimia 95%.
Mhe.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo Agosti 16, 2022, ikiwa ni siku sita tu baada
ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Comrade Daniel Chongolo kutoa
maelekezo, juu ya kiwanda hicho kwamba kitakapoanza uzalishaji wa majaribio
Septemba mwaka huu, kiendelee kupokea na kuchakata Chai moja kwa moja.
Pofesa
Ndalichako amesema “Kimsingi kiwanda kimekamilika kwa asilimia 95%, nimefanya
ukaguzi kwenye eneo la kupokelea na kuchambua Chai, eneo la kuichakata
(Processing), eneo la kuangalia viwango na ubora (Grading), eneo la Karakana, Tanuri
la kufua joto(Boiler) na kote huko kumekamilika.” Alisema.
Baada
ya kupokea maelekezo Waziri alisema wao kama Wizara alikaa na Katibu Mkuu pamoja
na Watendaji Wakuu wa Mifuko ya Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao ndio wawekezaji wakuu kwenye
kiwanda hicho ili kuona namna bora ya kuanza utekelezaji mara moja.
“Kulikuwa
na baadhi ya vifaa ikiwemo mabomba ya kutolea mvuke na nyavu za kukaushia chai ambavyo
vilihitajika ili kukamilisha hatua za uzalishaji.” Alifafanua.
Alisema
Kiwannda cha Chai Mponde kinakwenda kuwa kiwanda cha ksiasa na kitakuwa na
uwezo wa kuchakata tani 5,800 na baadaye uzalishaji utafika tani elfu 16,000.
“Kwa
siku wakulima watauza kilo elfu 52,000, naamini kwamba kiwanda kitaenda
kuinyanyua Halmashauri yetu ya Bumbuli na kuboresha maisha ya wananchi.” Alisema.
Mhe.
Profesa Ndalichako ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary
Mgumba, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalist Lazaro, Mkurugenzi Mkuu wa WCF,
Dkt. John Mduma mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Marco Kapinga, Mwenyekiti
wa Bodi ya Kiwanda hicho, Bw. Anselim Peter, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai na watendaji wengine wa kiwanda, alisema
kiwanda hicho kitatengeneza ajira za moja kwa moja 79 na zingine 100 hadi 200
kulingana na msimu wa kilimo.
“Niwahakikishie ndugu zangu wa Bumbuli, huu
ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, lakini pia ni utekelezaji wa nia njema ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua
wakulima.” Alisema Profesa Ndalichako.
Ameongeza
kwa namna yoyote ile kiwanda hicho ni kipaumbele katika Wizara anayoisimamia na
dhamira kubwa ni kuhakikisha ifikapo Septemba mwishoni kiwanda kianze kazi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba aliwahimiza wakulima wa
Chai kuanza uzalishaji wa Chai kwa wakati kwani kiwanda kinaanza kazi mapema kama
ambavyo imeelekezwa.
“Sisi
watu wa Tanga, watu wa Bumbuli na hasa Lushoto, uchumi wetu mkubwa unategemea Chai.
Tangu kiwanda kilipofungwa mwaka 2013, uchumi umedumaa na ushahidi ni mapato ya
Halmashauri ambayo si ya kuridhisha.” Alisema.
Aidha
wakulima wa Chai wameonyesha matumaini makubwa kufuatia ziara ya Mhe. Waziri
Profesa Ndalichako ambapo baadhi walifuatana nae kutembelea na kukagua
maendeleo ya kiwanda hicho.
“Mimi
sasa nina matumaini makubwa kwamba kiwanda hiki kitaanza kazi, nimeona
mabadiliko makubwa yamefanyika, nimshukuru sana Mhe. Rais wetu, Mama Samia
Suluhu Hassan kwa kazi kubwa hii iliyofanyika.” Alisema Mkulima wa Chai Bumbuli
Mzee Said Ngereza.
“Sisi
kama wakulima tumejipanga kwenda shambani, pelekeni salamu kuwa serikali
inatufungulia kiwanda nasi tuko tayari.” Alisema mkulima mwingine Bw. Shemdoe.
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako (Watatu kulia), akiangalia Chai iliyochakatwa wakati w
amajaribo ya awali ya kiwanda cha Chai Mponde alipokitembeela leo Agosti 16,
2022 ili kuona maendeleo ya ukarabaki wa kiwanda hicho kinachomilikiwa kw aubia
kati ya WCF na PSSSF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (Wapili kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea na kukagua kiwanda cha Chai Mponde Agosti 16, 2022. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba na katikati ya Mhe. Waziri na Mhe. Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma.