Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Injinia Ladslaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mawakala wa Tiketi za Ndege jengo la Amani Place jijini Dar es Salaam leo kuhusu ushirikiano wa Chama hicho na ATCL.
Bw. Moustafa Khataw Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Tiketi za Ndege Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Skylink Travel Agency akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Injinia Ladslaus Matindi kushoto na Bw. Moustafa Khataw Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Tiketi za Ndege Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Skylink Travel Agency wakipongezana mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
………………………………………
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) wanatarajia kuendelea kupanua huduma zao kwa kuanzisha safari ndani ya Bara la Afrika na Nchi za Ulaya ili kuwafikia wateja wengi zaidi.Safari zinazotaraji kuanzishwa ni za Nigeria,Ghana, Kinshasa -Congo na safari za Moja kwa moja London,Uingereza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara kwa wauzaji bora 20 wa tiketi za Air Tanzania ,Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alisema watahakikisha safari za China zitarejea huku za India zikiendelea kufanya vizuri.
“Tutatumia ziara hii kuboresha safari zetu na kujiandaa kwa upanuzi tayari tunaangali hili baada ya kufanya vizuri katika soko la Kongo kwenye kituo cha Lubumbashi tunaangalia mwaka kesho tutakapokuwa na ndege nyingine zaidi tutaingia kwenye soko la Goma na Kinshasa.Aliongeza
“Tunategemea Kwenda Afrika Magharibi tutaanza na Nigeria na Ghana tunapoingia lazima tuhakikishe hawa abiria wanapokuja wanakuja kwaajili gani kama wanakomea hapa au kuunganisha, safari za Afrika Kusini zinarudi lakini tunaanzisha safari ambazo zitavuti kutumia Air Tanzania kuunganisha safari zao hasa Ulaya huko London tutaenda kikanda na kimataifa,”alisisitiza.
Matindi alisema pia wataangalia safari za ndani kwani kuna mwitikio mkubwa kwa baadhi ya maeneo hivyo wataongeza idadi ya safari mara mbili hadi tatumaeneo kama Songea,Mpanda ambazo walianza na kisi cha chini.
Aliwashukuru mawakala kwa kuendelea kuwa sehemu ya biashara,kujadiliana ili kuona maboresho yaliyofanywa kwa jicho lingine la uhakiki zaidi na kuanza kuelezea mipango yao wa utanuaji wa mtandao wa safari.
“Wametoa mchango wametueleza mengi na tumewaeleza mengi kusaidia kurekebisha ,changamoto walizokutana nazo lakini na sisi kama wadau tumeeleza changamoto zetu ambazo wateja wametueleza ,tumezungumza kuhusu huduma,uuzaji wa tiketi ,mitandao yetu ,bei za tiketi ,ratiba zetu kila wakala alikuwa na maoni yake na sisi pia wamekuwa wawazi,”alieleza Alisema wamezungumza namna ya kuongeza idadi ya marubani ,wahandisi kwani ni changmoto namna ya kupata vipuri kwa wakati uonatakiwa .
“Changamoto kubwa ni mfano soko la India ni ule muunganisho wa safari Air Tanzania inashirikiana na Air India hivyo tiketi ni moja wanasema mara nyingi mfumo wetu zinakuwa hazisomi tumeliona na linafanyiwa kazi India ilikuwa inahamia kwenye mfumo mpya Kwa upande wake Mwenyekiti waw akala Tanzania ,Mmiliki wa skylink moja wapo waw akala ya tiketiMwenyekiti wa Mawakala wa Tanzania ,Moistafa Khataw alisema watashirikiana na ATCL kupata muafaka wa kupanua biashara ya Air Tanzania.
“Tumesisitiza kwamba kuna madhumuni maalumu ya kuzidisha vituo za Air Tanzania hasa zile za kimataifa ,tumeafikiana kuwa tutakuwa tunakutana kila muda flani ili kuzungumza kubadilishana mawazo kwaajili ya kazi zetu,”alibainisha.