Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na wanahabri jijini Dar es salaam leo kuhusu kuelekea Mbio za Hiari za Mwalimu Nyerere Marathon zinazotarajiwa kufanyika Oktoba mosi Mwaka huu.
Mwenyekiti na Mratibu wa Kamati ya Mwalimu Nyerere Adelaide Salhema akizungumza na wanahabri jijini Dar es salaam leo kuhusu kuelekea Mbio za Hiari za Mwalimu Nyerere Marathon zinazotarajiwa kufanyika Oktoba mosi Mwaka huu.(Picha na Mussa Khalid)
…………………….
NA MUSSA KHALID
Makumbusho ya Taifa la Tanzania Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Mbio za Hiari za Mwalimu Nyerere Marathon Ili kuendelea kuenzi na Kutangaza Urithi wa Muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema hatua hiyo ni sehemu ya program ya miaka 10 ya kumuenzi Muasisi Huyo wa Taifa lakini pia zinalenga Kuanzisha zao jipya la utalii kupitia Michezo.
Dkt Lwoga amesema kuwa Mbio hizo zinatarajia kufanyika Oktoba mosi Mwaka huu zikiwa na lengo la kutangaza urithi wa Mwalimu Nyerere Kitaifa na Kimataifa.
“Mbio za Hiari za Mwl.Nyerere (Mwl.Nyerere Marathoni) licha ya Kuanzisha zao jipya la utalii kupitia Michezo pia zinalenga kukusanya michango ya Fedha za Hiari kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Makumbusho na vituo vya Malikale vya Kumbukizi ya Mwl Nyerere ambao unaratibiwa na Makumbusho ya Taifa ambapo lengo ni kukusanya kiasi Cha Tsh Million Miatatu (300,000,000/-) kutokana na gharama za usajili WA wakimbiaji na wafadhili mbalimbali”amesema Dkt Lwoga
Aidha Dkt Lwoga amesema katika Mbio hizo Takriban washiriki 100 watashiriki ambapo kutakuwa na Mbio za Km 22 zenye washiriki 300,Mbio za Km 13 zenye washiriki 300,Km 4 zenye washiriki 200 ambao ni viongozi na watumishi Pamoja na washiriki wengine 200 ambao ni wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Dkt Lwoga amesema kuwa njia itakayotumika katika mbio hizo ni pamoja na barabara ya Butiama kwenda Busegwe kutokana na kuwa imebeba historia kwani Mwl Nyerere aliitumia kwenda shuleni wakati akioma shule ya msingi Mwisengi.
Kuhuru gharama za ushiriki wa mbio hizo Dkt Lwoga amesema ni Tsh 30000/- kwa watu wazima na Tsh 5000/- kwa wanafunzi ambapo wanatarajia zaidi ya watu 1000 kushiriki mbio hizo.
Kwa upande wake Mwenyekiti na Mratibu wa Kamati ya Mwalimu Nyerere Adelaide Salhema amesema maandalizi ya mbio hizo wameyafanya kwa kupata pia mwongozo kutoka Kamati ya Riadha ya Taifa.