Mkurugenzi wa miradi wa shirika la Children of Songea Shaban Tindwa wa pili kulia akikabidhi msaada wa solar kwa mtoto Shamsi Mustafa ili iweze kusaidia katika makazi yake,kulia mwakilishi wa shirika la Africa Power Richard Wallece.
Mkazi wa kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea Nasra Rajabu kushoto akipokea msaada wa solar kutoka kwa mkurugenzi wa miradi wa shirika la Children of Songea Shaban Tindwa uku mwakilishi wa kampuni ya KUWASOLAR Najumo Kipepe katikati akishuhudia.
baadhi ya wazazi na watoto wao wakijaribu kuunganisha vifaa ili kupata mwanga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa solar kwa kaya maskini katika kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea.
Shaibu Mussa na mama yake Mwanahid Shaibu wakihunganisha vifaa kwa ajili ya kupata mwanga baada ya kupata msaada wa solar uliotolewa na shirikala Children of Songea kwa kushirikiana na mashirika mengine ya KUWASOLAR na AFRICA POWER.
Mkurugenzi wa miradi wa shirika la Children of Songea Shaban Tindwa akizungumza na baadhi ya wazazi na watoto wa kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea baada ya kukabidhi msaada wa solar kwa kaya 115 zinazoishi mazingira magumu.
Baadhi ya watoto kutoka kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea,wakimsikiliza Mkurugenzi wa miradi wa shirika la Children of Songea Shaban Tindwa(hayupo pichani)kabla ya kupokea msaada wa umemejua(solar)ili uwasaidie katika makazi yao.
………………….
Muhidin Amri,Songea
SHIRIKA la Children of Songea kwa kushirikiana na wadau wengine shirika la Africa Power na Kuwasolar,wametoa msaada wa umeme jua(solar)kwa kaya 115 zinazoishi mazingira magumu katika kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea.
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa miradi wa shirika hilo Shaban Tindwa alisema,kwa muda mrefu wanatoa misaada kwa watu na familia zinazoishi katika mazingira magumu ili kuwafariji kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.
Alisema, gharama za solar hizo ni zaidi ya Sh.milioni 18 na mpango wa shirika la Children of Songea ni kuendelea kuwasaidia watoto hao ili wapate nafasi kubwa ya kusoma na hatimaye waweze kutimiza malengo yao.
Alisema, kwa mara ya kwanza wameanza kutekeleza mpango huo katika kata ya Ruvuma, na wamelenga hasa kaya zenye watoto wanaosoma shule za msingi na sekondari.
Tindwa alieleza, matumaini yao kuwa solar hizo zitawasaidia watoto wanaotoka kwenye kaya hizo kuongeza taaluma kwenye masomo yao kwa kupata muda mwingi wa kujisomea hasa nyakati za usiku.
Alisema,tangu mwaka 2015 Children of Songea inatoa vifaa vya shule,sale kwa wanafunzi,chandarua kwa watoto ili kuwakinga na ugonjwa wa malaria,kulipia bima ya Afya(CHF) kwa watoto wanaotoka kwenye kaya zinazoishi mazingira magumu na kukarabati nyumba.
Aidha alisema, kupitia mpango huo wamefanikiwa sana kuongeza hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kufanya vizuri darasani na hatimaye kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika shule mbalimbali hapa nchini.
Mwakilishiri wa KuwaSolar Najumo Kipepe alisema,lengo la msaada huo ni kusaidia kupata mwanga ambao utasaidia kuchagiza taaluma kwa wanafunzi na kujikwamua kiuchumi katika kaya hizo.
Kipepe, amewataka wazazi na walezi wa watoto hao kuhakikisha wanatunza solar hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na zisaidie kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili.
“ni furaha yetu kuona kila mmoja nafikiwa na umeme popote alipo kwa kuzingatia hasa umuhimu waw a umeme kwenye makazi yetu”alisema Kipepe.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la Africa Power Richard Wallec alisema,mara ya kwanza alipotembelea baadhi ya kaya hizo aliumizwa sana kuona hakuna mwanga wa kutosha kwenye nyumba zao licha ya kuwa ilikuwa majira ya mchana
Richard,amewashukuru wakazi hao kwa kumkaribisha katika jamii yao hali iliyomwezesha kufahamu baadhi ya changamoto na matatizo yanayowakabili na kuhaidi kuendelea kuzisaidia familia hizo
Mmoja wa wazazi Pilmina Hyera,ameyashukuru mashirika hao kwa msaada huo na kueleza kuwa, solar hizo zitawasaidia watoto wao kusoma nyakati za usiku na kuhaidi kama wazazi watahakikisha wanawasimamia watoto wao kusoma kwa bidii.
MWISHO.