NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MBEYA
MKURUGENZI
wa Huduma za Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Abdulsalaam Omar, amesema Maonesho ya
Nanenane mwaka huu 2022 yanayofanyika jijini Mbeya, yana maana kubwa kwa Mfuko
huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo alisema kaulimbiu ya Maonesho hayo
inayosema “Agenda 10/30 Kilimo ni Biashara; Shiriki Kuhesabiwa ili kutekeleza
vizuri Mipango ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi,” inaakisi moja kwa moja shughuli na mipango ya WCF
kwa maana hivi sasa kilimo hiki sio kile cha mazoeza kwani kinatarajiwa kuongeza ubora na kuthaminiwa kama ilivyo biashara zingine hili ni jambo kubwa la kukuza uchumi wa nchi nasisi WCF tunaipongeza sana Serikali ya Awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kama
ulivyosikia siku ile ya ufunguzi wa Maonesho haya, Serikali imedhamiria
kukifanya kilimo chetu kuwa cha Biashara, na ndio maana kauli mbiu inataja Kilimo
ni Biashara, kwa hivyo hapa unazungumzia ajira za wafanyakazi.” Alisema
Unapozungumzia
masuala ya ajira maana yake moja kwa moja WCF inaingia hapo kwa hiyo wote
walioajiriwa rasmi ni wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na pindi
wanapopatwa na changamoto za ajali au magonjwa yanayotokana na kazi wanapokuwa
wanatekeleza shughuli zao za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa namna moja ama nyingine
watastahili kulipwa fidia, alisisitiza Dkt. Omar.
“WCF
tuko hapa kukutana na Wakulima, Wafugaji na Wavuvi ili na wao waweze kujua haki
zao mbalimbali ikiwemo ni Mafao gani wanaweza wakapata na tunawakaribisha wananchi katika Banda la WCF.” alisema.
Alisema
kama ambavyo wamekuwa wakitekeleza jukumu la kulipa fidia kwa wafanyakazi
wanapoumia au kuugua kutokana na kazi kwa mujibu wa mikataba yao ya kazi, pia
wakulima,wafugaji na wavuvi nao watastahili kupata haki za kufaidika na Mafao
hayo kwa vigezo vile vile vinavyotumika.
Aliyataja
Mafao hayo kuwa ni pamoja na Fao la Matibabu, Fidia ya Ulemavu wa Muda, Mafao
ya Ulemavu wa Kudumu na yanaweza kuwa ya mkupuo au kulingana na kiwango inaweza kuwa pensheni ya kila mwezi, naendapo itatokea amefariki basi wale
wategemezi wake watalipwa fidia na Mfuko.
Kuhusu
viwango vya uchangiaji katika Mfuko, Dkt. Omar alisema hivi sasa Serikali imepunguza viwango vya michango kutoka
asilimia 0.6% kwenda asilimia 0.5 kwa waajiri walio katika sekta binafsi sawa
na wale wa sekta ya Umma.
Wakizungumza
baada ya kutembelea banda la WCF, wafanyakazi mbalimbali wameipongeza serikali ya awamu ya
sita chini ya uongozi wake Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuuwezesha Mfuko huo kuwahudumia wafanyakazi
wanapopatwa na changamoto mbalimbali wawapo kazini.
“Ni
jambo jema sana Mfanyakazi anapokuwa anatekeleza majukumu yake na ikatokea
amepata changamoto za kuumia, kuugua ama kufariki akiwa kazini aweze kupata
haki yake ya kufidiwa, ni kitu kizuri na ninampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kuuwezesha Mfuko huu kutekeleza majukumu yake.” Alisema Bw.
John Chazi ambaye ni Mfanyakazi kwenye Chuo Cha Kilimo Inyala, Mbeya.
Mfanyakazi
mwingine wa jijini Mbeya Bw. Aloyce Gonzaga alisema yeye amepata Elimu zaidi kwani alikuwa anausikia Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na aliamua kutembelea
banda la WCF ili kupata uelewa zaidi wa
namna gani mfanyakazi anaweza kufidiwa endapo atapata madhila yoyote akiwa
kazini.
Aidha
Afisa Mfawidhi wa WCF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi. Rose Satta ametoa wito kwa wafanyakazi kutoka sekta zote
walio katika ajira rasmi kwenye Kanda hiyo kutembelea Ofisi za WCF Kanda
zilizoko jijini Mbeya.
wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Bi. Laura Kunenge, akifafanua jambo wakati akitoa elimu kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi na shughuli za Mfuko huo kwa
Mfanyakazi huyu aliyetembelea banda la WCF kwenye Maonesho ya Nanenane viwanja vya
John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 7, 2022.
Afisa Mfawidhi wa WCF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi. Rose Satta (kushoto), akitoa elimu ya fidia na shughuli zinazotekelezwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Nanenane viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 7, 2022.
Satta akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Profesa Mkumbukwa Angelo Mtambo, (kushoto) alipotembelea Banda
la WCF. Kulia ni Afisa wa WCF, Bi. Aruna Mwakanyamale.