Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule akizungumza katika mahojiano maalum na Kituo cha habari cha Chanel 10 katika Banda lao kwenye Mzonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefulewa (wa tano kutoka kushoto na kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika hilo katika maonesho hayo.
………………………………………
NA JOHN BUKUKU MBEYA
Maonesho ya Kilimo Nanenane mwaka huu yamekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa Jiji la Mbeya na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla kutokana na ushiriki wa taasisi na makampuni mbalimbali nchini ambapo Shirika la Bima la Taifa (NIC) pia limeweka kambi katika Maonesho hayo huku likiwa na kikosi kazi kamili kutoka katika Idara tofauti na kikiongozwa na Idara ya Masoko.
Ushiriki wa NIC kwenye maonesho haya unatoa fursa kwa wananchi wanaotembelea hususani wadau wa kilimo na mifugo kufahamu huduma za Bima mbalimbali zinazotolewa na Shirika letu ikiwemo Bima ya mazao ambayo imekuwa mkombozi kwa wakulima hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Yessaya Mwakifulefule msimamizi nguli wa masoko nchini wakati akihojiwa na waandishi wa habari katika mahojiano maalum yaliyofanyikai katika Banda la Shirika hilo.
Mwakifulefule amesema Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali juu ya huduma za Bima wanazozitolewa kwa wananchi wanaotembelea katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John Mwakangale Jijini mbeya ili kuwapa ufahamu zaidi juu ya huduma za shirika hilo na faida zake.
“Tupo hapa kwenye maonesho ya Nanenane tunataka watanzania wote kwa ujumla kufahamu Huduma zetu za Bima, kwa wakulima wakubwa kwa wadogo pamoja na wafugaji ilimradi tu awe ana shamba lake kuanzia heka moja kwenda juu waje wakatie Bima mazao yao na mifugo yao ili ikitokea wanapata majanga waweze kulipwa fidia zao. Hakuna haja ya kuwa na hofu kama ni kuharibika kwa mazao au kufa kwa mifugo NIC ipo tuletee sisi hizo ‘Stress’ zako za kibiashara tukae nazo sisi wewe baki na maisha ya amani” amesema Mwakifulefule.
Amesisitiza kuwa Shirika hilo limeendelea kujiimarisha katika kuwafikia wakulima wengi kwa kuwapa elimu juu ya uwepo wa Bima hiyo ambapo amebainisha uwepo wa kikosi kipana cha vijana wenye weledi na ujuzi mkubwa katika kutoa huduma za Bima pamoja na timu nzima ya elimu na masoko kwa umma iliyowezesha kuwafikia wananchi wengi kufahamu Huduma zao.
Amesema mwamko ni mkubwa sana kwa vijana kujihusisha na kilimo na NIC inaungana na Serikali katika kuhakikisha vijana wanaungwa mkono kwenye jitihada za kuwahusisha katika kilimo.
“Tumemsikia Mhe. Waziri Mkuu akisisitiza kuwafikia vijana wengi, na sisi tuko tayari kuwafikia na kuwahamasisha huku tukiwaelimisha juu ya Bima hii ya mazo ili wawe na uhakika wa kazi zao za kilimo na ufugaji kwani sisi ndiyo BIMA,”. amesema Mwakifulefule