Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa kwa watoto wanaolazwa katika Taasisi hiyo wakati wajumbe hao walitembelea wodi ya watoto ya JKCI.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiwaeleza wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo jinsi upasuaji wa moyo kwa watoto unavyofanyika. Wajumbe hao walitembelea maeneo mbalimbali ya JKCI kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Daktari wa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Iddi Makapu akiwaeleza wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo huduma zinazotolewa katika chumba hicho walipotembelea ICU kabla ya uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo.
Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Menejimenti ya Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipofika katika taasisi hiyo leo jijini Dar ea Salaam kwaajili ya kuzindua Bodi ya Wadhamini ya JKCI.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizindua bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akimkabidhi begi lenye vitendea kazi mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kuizindua bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.