Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) limetoa mwito kwa wajasiriamali hususani wanaojihusisha na kilimo na bidhaa za usindikaji kujihepusha na watu wanaotoa mafunzo mitaani na badala yake kufika katika vituo vya SIDO vilivyoeneoa nchi nzima ili kupata mafunzo sahihi na kuweza kufikia malengo yao kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Meneja Masoko wa SIDO Lilian Massawe amesema kuwa lengo la wao kushiriki katika maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya teknolojia ya viwanda vidogo itakayowawezesha kupata tija katika shughuli zao.
Amesema kuwa katika maonesho hayo wamekwenda na wahjasiriamali mbalimbali waliopata mafunzo kupitia Shirika hilo na kwamba wananchi wanakaribishwa kutembelea katika banda hilo.
Picha mbalimbali zikionesha wajasiriamali wakiendelea na shughuli za maonesho Katika Banda la taasisi hiyo.