KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo amesema kuwa, kazi ya Serikali ya CCM ni kutafuta njia za kutatua changamoto za wananchi na sio porojo.
Chongolo alitoa kauli hiyo tarehe 2 Agosti, 2022 alipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya na nyumba za watumishi katika kijiji cha Chekimaji kata ya Masama wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu amefurahishwa na namna serikali inavyoendelea kukatua changamoto za wananchi ambapo amesema kuwa, kazi ya Serikali ya CCM ni kutafuta njia ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na sio vinginevyo.
Amesema kuwa, hawategemei kuona Serikali ikipiga porojo wala ikikunja nne wakati wananchi wanapata shida na pindi wananchi wanapolalamika jukumu la Serikali ni kulitafutia ufumbuzi wa jambo linalolalamikiwa.
Hili limeonekana baada ya wanananchi wa kata ya Masama kuonesha wanauhitaji wa zahanati ambapo walichangisha fedha milioni 11 na kuanza ujenzi Serikali iwaunga mkono kwa kutoa fedha milioni 590.
Ambapo Katibu Mkuu amedokeza kuwa, “Moja ya changamoto ya kubwa tulionayo ni kulaumu, tunasubiria mambo mabaya yatokee tulaumu lakini pale ambapo Serikali na watumishi wake wanapofanya mambo mazuri kulingana na Ilani hatuwapongezi ni lazima tujenge utamaduni wa kupongezana pale tunapoona mambo mazuri ilikuendelea kutiana moyo” amesema Katibu Mkuu.
Amesema kuwa, tabia ya kusubiri kulaumu na kuchongeana na kutengenezeana nongwa kwenye mabaya tu sio vizuri kwani Binadamu sio malaika, tunakosea.