Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani Idara ya uhamiaji imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kijamii kuwa idara hiyo inapokea malipo mkononi kutoka kwa wateja wakati inafamika malipo yote ya serikali hulipwa kwa njia za huduma za kifedha.
Kamanda wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha Mratibu msaidizi Samwel Mahirani ameyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake na kuwataka watanzania kuwaamini viongozi wao na kutoa taarifa za malalamiko bila woga
Amekemea vikali wale wote wanatumia mtandao kuichafua Idara hiyo kuacha mara moja na pia kutoa taarifa kwa uongozi pindi wanapoona hawa kuridhishwa na huduma kwani kuna vitengo mbali mbali na box la maoni haoni sababu ya kulizungumza mtandaoni.
“Taasisi zote za umma hazipokei fedha mkononi bali fedha zote za umma zinapokelewa kwa njia ya miamala ya kifedha ikiwemo benki na mitandao ya simu za mkononi” alisema Kamanda
Alisema kuwa Hapendezwi na wanaotumia mitandao ya kijamii kuichafua Idara hiyo kwa kusema wanachukuwa rushwa na kupokea fedha mkononi hilo sio sahihi walitakiwa kufika ofisini kwangu na wakiona hawawezi kuniona basi kuna taasisi za kupambana na kuzuia rushwa badala ya kukimbilia huko.
Amesema Idara hiyo mwaka 2018 wamefanya misako na doria Zaidi 234 na kukamata wahalifu 96 waliofikishwa mahakamani ambapo 128 kutoka mataifa mbali mbali waliondoshwa nchini
Amebainisha kuwa Jumla ya Pasi kubwa za kusafiria 1384 zimetolewa tokea Dec hadi mei mwaka huu sanjari na pasi ndogo 14,183 ambapo idara ya uhamiaji mkoani hapa imezitoa kwa wananchi wanaosafiri nje ya nchi.
Alieleza kuwa wahalifu 314 kati yao 38 walipandishwa mahakamani ambapo 86 waliondoshwa nchini ambapo Idara hiyo imetoa angalizo kwa askari wake wenye tabia hizo kuacha mara maja kwani.
Akatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo viovu na kuacha kutumia mitandao ya kijamii ili na wao kuweza kuboresha huduma zao kwani maoni yanasaidia kuliko kutoa malalamiko kwani hayajengi.