********************************
Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosailia ya
mahakama za makosa ya jinai, leo imeanza kusikiliza shauri la
aliyekuwa waziri wa mipango wa nchini Rwanda Augustin Ngirabatware
aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa matano likiwepo la
kuhusika na mauaji ya Kimbari.
Shauri lililosomwa katika mahakama hiyo iliyopo Arusha kaskazini mwa
Tanzania , pamoja na mambo mengine linaeleza kuwa watu waliotoa
ushahidi dhidi ya Ngirabatware walishawishiwa ili waseme uongo
mahakamani.
Mmmoja wa mashahidi hao ameiambia mahakama leo kuwa wakati anatoa
ushahidi miaka 10 iliyopita, alikuwa amehukumiwa kifungo cha kunyongwa
na hivyo alishawishiwa atoe ushahidi wa uongo mahakamani ili
apunguziwe adhabu.
Mwaka 2012, Ngirabatware alihukumiwa kifungo cha miaka 35 Jela na
mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda baada ya
kukutwa na hatia ya kuhusiaka katika mauji ya kimbari kwa kushirikiana
na kundi la mauaji ya halaiki la nchini humo Interahamwe , pamoja na
kosa la ubakaji.
Mwaka 2014, Mahakama ya rufaa ya Rwanda ilimpunguzia adhabu ya kifungo
kutoka miaka 35 hadi 30 baada ya kuondoa kosa la ubakaji ,kifungo
ambacho anakitumikia hadi leo.
Hukumu ya kesi ya Ngirabatware inatarajiwa kutolewa tarehe 27 ya mwezi huu