Mwenyekiti wa Umoja wa kikundi cha ‘Nkelei na Mabadiliko’,Kassim Kipingu akizungumza katika mkutano maalum wa kikundi hicho ambacho kimefanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanaumoja huo wa kikundi cha Nkelei na Mabadiliko waliohudhuria Katika mkutano huo.
……………………….
NA MUSSA KHALID
Umoja wa kikundi cha wanakijiji Cha Nkelei kilichopo Kata ya Rangwi,Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga umesema unatarajia kuzindua Shule ya Sekondari na Zahanati ambazo zimejengwa kwa Nguvu ya Umoja huo kwa kushirikiana na serikali siku kadhaa zijazo.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es alaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambao wameupa jina la ‘Nkelei na Mabadiliko’,Kassim Kipingu wakati akizungumza katika mkutano maalum wa kikundi hicho ambacho hufanya kila mwisho wa Mwezi.
Kipingu amesema chama hicho kimekuwa na sura Mpya na nzuri kwani wamefanikiwa kujenga majengo hayo mpaka hatua iliyofikia na kueleza kuwa wakikamilisha itasaidia kuondoa adha iliyokuwa inawakabili wanakijiji hao Kwa kwenda umbali mrefu kutafuta huduma.
Amewataka wanaumoja huo kuendelea kuonyesha Umoja wao katika kikundi hicho Ili kuendelea kufanikisha zaidi malengo waliyojiwekea.
“Mpaka Sasa tunajivunia Umoja wetu huu Kwa sababu tumetembea na miradi hii miwili ya Shule ya Sekondari Nkelei na Zahanati ambazo zipo kwenye hatua ya Mwisho”amesema Kipingu
Aidha amesema licha ya dhamira ya kikundi hicho kuanzishwa kwa lengo la kusaidiana shida na matatizo mbalimbali ikiwemo kunapotokea misiba, wamefanikiwa kufanya maendeleo kujenga majengo mawili yenye madarasa manne ambapo Kwa sasa wanachosubiri ni zoezi la Choo kukamilika Ili Shule hiyo iweze kufunguliwa.
Amewataka wanaumoja huo kuendelea kuogeza juhudi na jitihada katika kuonyesha thamani ya kwao walipotoka Ili kuyafanikisha maendeleo.
Mwenyekiti Huyo pia ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya Wilaya akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mlalo Rashid Shangazi kwa kuwaunga Mkono Katika kufanikisha Ujenzi wa miradi hiyo.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa Kamati ya Maendeleo ya Nkelei Omary Waziri amesema wa kushirikiana na viongozi wa Wilaya hiyo wamesaidia kufanikisha hatua hiyo kuifikia.
Amesema Hali ya Maendeleo inaendelea vizuri hivyo amewataka wanaumoja huo wa Nkelei na Mabadiliko kuendelea kuongeza hamasa zaidi kwa kuendelea kutoa mchango wao Pindi itakapohitajika.