Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano makatibu wakuu na maofisa waandamizi wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano makatibu wakuu na maofisa waandamizi wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia jijini Dar es Salaam.
………………………………………………
NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zipo katika mkakati wa kuwa Mfumo Satelaiti ambapo utawezesha taarifa za nchi hizo kudhibitiwa katika ukanda huo bila kuvuka mipaka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ufunguzi wa mkutano makatibu wakuu na maofisa waandamizi wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia jijini Dar es Salaam.
Waziri Kamwelwe alisema kwa muda mrefu nchi za SADC zimekuwa zikitumia mfumo wa Satelaiti ambao unahitaji taarifa kwenda katika nchi za Ulaya na Marekani ndio zirudi nchini na kumfikia muhusika hivyo wanataka kuondokana na utaratibu huo.
Alisema maofisa hao waandamizi watatumia mkutano huo kujadili na kuja na ubunifu ambao utarahisisha kila nchi mwanachama kusimamia mawasiliano yake bila kutegemea uthibiti kutoka nje ambao sio salama kwa nchi na watuamiaji.
“Mkutano huu huu wa siku tano wa sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni mwanzo mzuri wa nchi za SADC kuweka mazimgira salama katika mfumo wa ke wa taarifa na mawasiliano ya inteneti kwani tupo kwenye mkakati wa ujenzi wa Satelaiti ya pamoja hivyo kuachana na mifumo ya zamani,” alisema.
Mhandisi Kamwelwe alisema kukamilika kwa mfumo huo wa kutumia Satelaiti moja kutapunguza gharama za inteneti ambazo kwa sasa ni kubwa hivyo ni matumaini yake kuwa wataalam hao watakuna vichwa katika eneo hilo.
Alisema iwapo mfumo huo wa kutumia Satelaiti moja utafanikiwa utaweza nchi wanachama kusaidiana kupata taarifa kwa pamoja huku usalama ukiwa mkubwa zaidi.
Aidha, alisema mkutano huo utajadili masuala ya majanga kwa nchi husika ili waweze kuwa na mipango ambayo inaweza kutatua changamoto hiyo ili isilete madhara makubwa.
“Mwaka jana kulikuwa na mvua kubwa katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi lakini kukosekana kwa mifumo rasmi ya kutoa taarifa kwa pamoja hupelekea nchi husika kujiandaa namna ya kukabiliana na hali hiyo,” alisema
Alisema vijana ambao wanasomeshwa na nchi za SADC katika sekta ya majanga na uhandisi kwa ujumla wanapaswa kutumika kulinda usalama wa nchi zao kukabiliana na majanga.
Waziri Kamwelwe alisema Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wamebuni njia mbili ambazo zimekubalika duniani hivyo wataalam wakikaa pamoja wanaweza kusaidia nchi za SADC kutatua changamoto zake.
Alisema waatalam hao watajadiliana na kuja na mapendekezo ya kitaalam kuhusu miradi ya usafirishaji na uchukuzi ambayo itapaswa kutekelezwa kwa nchi zote wanachama.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena alisema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mokoena alisema baadhi ya nchi zimeonesha uthubutu katika ujenzi wa miundombinu akitolea mfano wa Tanzania hivyo kuzitaka nchi zingine ziongeze jitihada katika eneo hilo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wan chi husika.
“SADC ina program yake ya kuendelea miundombinu katika sekta zote hivyo mkutano huu ni mwanzo mzuri wa utekelezaji huo ni imani yangu kuwa tutaweza kufikia mazimio yenye tija kwa kila nchi mwanachama,” alisema.
Mkurugenzi huyo ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa SADC, Dk.Stergomena Tax alisema sekta ya Tehama, Bahari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni sekta muhimu katika kukuza uchumi hivyo ni vema kila nchi kuwekeza katika eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard Chamriho akimkaribisha waziri Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ikilikufungua mkutano huo.
Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa pamoja na wajumbe wengine wakiwa katika mkutano huo leo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano.
Waziri Isaack Kamwelwe akiwa na viongozi mbalimbali meza kuu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Picha ya pamoja ya mwaziri wa SADC na wajumbe wa mkutano huo.