Baadhi ya Wachezaji wakiwa wamevalia Jezi za Ugenini Nyeusi na Nyumbani Za Kijani wakizionyesha kwa Wadau katika Hafla iliyofanyika Club 361 Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kombania ya Muziki Meja Nimroad Kitinya akipokea Udhamini wa Jezi kutoka Kwa Mwakilishi wa Smart Gin Forgiver Tito wakati wa Sherehe ya Uzinduzi wa Jezi mpya za Timu ya Green Warriors inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza katika hafla iliyofanyika Club 361 mwenge Jijini Dar Es Salaam.
****************************
Wachezaji wa Timu ya Green warriors inayomilikiwa na JWTZ inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza wametakiwa kujituma kuhakikisha wanapanda Ligi kuu kwani Uwezo wanao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kombania ya Bendi Meja Nimrod Green Warriors wakati wakitambulisha jezi za msimu wa Mwaka 2019/2010 Club 361 Mwenge Dar es Salaam.
KLABU hiyo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza (FDL) imetambulisha jezi za msimu na mdhamini wao mpya huku ikihimizwa kuhakikisha inapambana uwanjani ili kupata Mafanikio kwani kuifunga simba ni ishara uwezo wanao.
Timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2000 imechagua jezi ya kijani kuwa ya nyumbani na nyeusi ya ugenini katika utambulisho huo uliofanyika juzi usiku ambapo pia walikabidhiwa rasmi vifaa vya michezo na mdhamini wao Smart Gin tayari kwa kuanza msimu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jezi hizo Nimrod Kitinya kwa niaba ya Mlezi Mkuu wa kambi Makao Makuu ya Jeshi alisema Warriors ni timu kubwa kwa sasa hivyo, ni lazima ikaonyeshe ushindani wa kweli na jitihada ili kufikia lengo la kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
“Green Warriors ni timu kubwa kama iliweza kuwafunga Simba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho kwanini isipambane kupanda Ligi Kuu ? Mjitahidi kupeperusha vyema bendera ya Jeshi kutimiza lengo, “alisema.
Naye mdhamini wao ambaye ni mwakilishi wa masoko wa Kampuni ya Euromax chini ya kinywaji cha smartgin Forgiver Tito alisema wamejitokeza kuiunga mkono timu hiyo baada ya kugundua klabu nyingi zimekuwa zikipata wakati mgumu kwa kukosa udhamini hali inayodhoofisha ushindani.
“Kama mdhamini tumeona mapungufu na kubwa ni Ligi ya daraja la kwanza kukosa udhamini. Rai yangu kwa makampuni mengine wajitokeze kudhamini timu hizi kwani ndiko ambako vipaji vingi vinazaliwa na kulibeba taifa baadaye , “alisema.
Mmoja wa wadau wa klabu hiyo Selemani Semunyu aliwapongeza Smart Gin kwa kuiwezesha klabu hiyo vifaa vya michezo na kutaka wachezaji kufanya vizuri katika mechi zao ili kuwatia moyo wadhamini .