Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus Lumato (kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Julai 16,2022 Jijini Dar es Salaam kilicholenga kufahamiana na kubadirishana mawazo kwa pamoja ambapo pia Mkurugenz huyo amezungumzia matumizi ya Gesi kwenye magari na majumbani na kupanda kwa Bei ya mafuta. (kushoto aliyekaa) ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto aliyekaa) akipiga makofi kupongeza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus (kulia anaezungumza) wakati alipokuwa akizungumza katika Kikaokazi hicho.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo akizungumza kwenye kikao hicho alipokuwa akiwakaririsha wahariri wa vyombo vya habari (hawamo pichani) kwenye kikao hicho kilichofanyika leo Julai 16,2022 Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Huduma kwa wateja wa EWURA Kanda ya Mashariki Getrude Mbiling’i akifuatilia mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea kati ya EWURA na wahariri hao.
Na: Thobiesa Makafu.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar.16/07/2022, imekutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari chini ya Jukwaa la Wahariri (TEF) nchini ili kujadili masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Modestus Lumato alisema, “wahariri wa vyombo vya habari wana jukumu muhimu sana katika kuhabarisha jamii, hivyo mkutano huu unalenga kujadiliana na kuongeza uelewa juu ya sekta zinazodhibitiwa pamoja na kupokea maoni na ufafanuzi juu ya masuala ya kiudhibiti”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Bw. Deodatus Balile ameeleza, wahariri wataendelea kushirikiana na EWURA katika utekelezaji wa shughuli za udhibiti kwa maslahi mapana ya watanzania.
“EWURA inathamini mchango wa tasnia yetu ya habari, nasi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kila wakati”
Akitoa neno la shukrani, Mwandishi mkongwe Salim Salim ameeleza kuwa, kazi zinazofanywa na wahariri pamoja na waandishi wa habari nchini, ni utekelezaji wa wajibu wao hivyo watatumia nafasi walizonazo kuhakikisha wananchi wanaelewa masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji.