****************************
NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ametengua katazo la halmashauri ya mji wa Njombe lililopiga marufuku mabasi ya abiria kushusha abiria katika ya mji kwa madai ya kwamba katazo hilo linawaumiza wananchi wa hali ya chini.
Mei 11 mwaka huu halmashauri hiyo ilianza kutumia kituo kipya cha mabasi kilichojengwa kwa ufahadili wa benki ya dunia uliagharimu zaidi tya bil 9, ambapo katika uzinduzi huo halmashauri ya mji wa Njombe ilipiga marufuku mabasi ya abiria yaendayo mikoani na vijijini kushusha abiria katika vituo viliyopo katikati ya mji jambo ambalo limesababisha kuibuka kwa malalamiko mengi kwa wananchi kwasababu ya umbali wa kituo kipya cha mabasi.
Akitengua marufuku hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi mkuu wa mkoa wa Njombe Olsendeka amesema kuwa maamuzi hayo yamewafanya kutumia fedha nyingi wananchi kukodi tax na boda boda hatua ambayo imesababisha chuki dhidi ya wananchi na serikali hivyo anatengua katazo hilo na kuitaka halmashauri hiyo kuketi tena ili kuweka mkakati wa kukifanya kituo kipya kuwa hai bila kuathiri wananchi.
Wakati akitengua katazo hilo Olesendeka ili kukifanya kituo hicho kuwa hai muda wote mabasi ya abiria yaliokuwa yakilipa shilingi elfu moja kila linapo ingia kituo kipya cha mabasi yataanza kulipa elfu mbili
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amesema ili kuwapunguzia changamoto ya usafiri atatengeneza kwa gharama zake kituo kidogo cha kushusha abiria jirani na hospitali tegemeo ya mji wa Njombe Kibena ili magari ya abiria yawe na uwezo wa kushusha abiria ambao wanaenda hospitalini hapo kupata matibabu.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Njombe akiwemo Rose Mayemba na Edmund Nziku wametoa hisia zao kuhusu kufutwa kwa marufuku hiyo wakidai kwamba hali ilikuwa ngumu kwa kuwa kuna baadhi ya mitaa wananchi walilazimika kutumia kuanzia shilingi elfu tano hadi kumi kukodi bajaji,boda na tax ili kufika kituo kipya cha mabasi kilicho kata ya mji Mwema .
Takriban miezi sita imepita tangu kituo kianze kutumika huku kikiwa na malalamiko lukuki ya wananchi.