Waziri Mstaafu wa Ardhi Nyumba na Makazi  Profesa Anna Tibaijuka  akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusisono wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw, Geofrey Meena leo wakati  alipotembelea banda la STAMICO  na kukutana wachimbaji  wadogo waliokuja katika maonesho hayo.
Akiongea  baada ya kutembelea  mabanda yote Prof. Tibaijuka amesema amefurahishwa na uthubutu wa wachimbaji hao katika maonesho 
Ameipongeza STAMICO kufuatia hatua za kuwasaidia   kupata mikopo na kuwataka wachimbaji kushirikiana na  STAMICO katika utafutaji wa Mikopo  kutoka taasisi  za fedha zenye  unafuu ili waweze kufanya uchimbaji wenye tija.
Wadogo  wanahitaji mikopo nafuu, ni vyema  pia wakaangalia namna ya kuishirikisha benki ya TIB  ili iweze kuwanufaisha  wachimbaji.
Sambamba na hilo amefurahishwa na ubunifu wa mkaa Mbadala  ambao  ni njia moja wapo ya kuzuia uharibifu wa mazingira.

Waziri Mstaafu wa Ardhi Nyumba na Makazi  Profesa Anna Tibaijuka akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusisono wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw, Geofrey Meena kulia ni Bw. Oto kutoka STAMICO na Kushoo ni Bibiana Ndumbaro Aisa habari wa STAMICO.

Waziri Mstaafu wa Ardhi Nyumba na Makazi  Profesa Anna Tibaijuka akipata maelezo kutoka kwa Eric Ketagory Afisa Usimamizi wa Fedha TEITI wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo.

Bw. Osman Abdulsattar  Tharia Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Mineral Dealers Association akimkabidhi zawadi Profesa Anna Tibaijuka wakati alipotembelea banda la STAMICO katikati ni  Meneja Masoko na Uhusisono wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw, Geofrey Meena

Meneja Masoko na Uhusisono wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw, Geofrey Meena akimkabidhi zawadi mkaa mbadala Profesa Anna Tibaijuka mara baada ya kutembelea banda la STAMICO leo.

Profesa Anna Tibaijuka akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wanaofanya kazi maalum katika banda la STAMICO mara baada ya kutembelea banda hilo leo.

Profesa Anna Tibaijuka na Meneja Masoko na Uhusisono wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO Bw, Geofrey Meena wakiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wafanyakazi wa STAMICO   mara baada ya kutembelea banda la STAMICO leo.