NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SABASABA
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu), Profesa Jamal Katundu amewakumbusha waajiri kote nchini kujisaliji
kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kuwasilisha michango kwa wakati
kwani kufanya hivyo watakuwa wametekeleza haki ya msingi ya mfanyakazi kufidiwa
pindi anapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Profesa
Katundu ametoa wito huo Julai 8, 2022 baada ya kutembelea banda la WCF kwenye
Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya
Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam.
“Ni
haki ya msingi ya mfanyakazi, kwa mwajiri wake kujisajili kwenye Mfuko wa WCF na
kuhakikisha kwamba michango anawasilisha kwa wakati ili malengo yaliyokusudiwa ya
kuanzishwa kwa Mfuko yaweze kutekelezeka.” Alifafanua Profesa Katundu.
Alisema
amefurahishwa na jinsi watumishi wa WCF wanavyotoa huduma kwa wananchi kwani
kila dawati alilopita ameona jinsi wananchi wanavyohudumiwa kwa kupatiwa elimu
na ufafanuzi mbalimbali kuhusu masuala ya fidia na shughuli za Mfuko kwa ujumla
wake.
Miongoni
mwa huduma zitolewazo kwenye banda la WCF lililoko mtaa wa Mabalozi, ni pamoja
na elimu kuhusu jinsi ya kujisajili na Mfuko kwa kutumia Mifumo ya kisasa ya
TEHAMA, kuwasilisha michango, jinsi ya kutoa taarifa pindi mfanyakazi
anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi, lakini pia jinsi tathmini ya ulemavu
inavyofanyika, alisema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Umma, WCF Bi.
Laura Kunenge.
“Tumejipanga
kuhakikisha tunawahudumia wateja wetu ( waajiri, wafanyakazi na wananchi kwa
ujumla) kuhusu uelewa wa jumla wa Mfuko na huduma zetu tunazotoa hapa ni kama
zile zinazopatikana kwenye ofisi zetu za Makao Makuu na Kanda.” Alifafanua.
Kaulimbiu
ya mwaka huu ya Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28 na yanayotarajiwa kufikia
kilelel Julai 13, 2022, ni “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara ya Uwekezaji.”.
Profesa Katundu (kulia) akipokea majarida ya WCF na nembo ya Mfuko kutoka kwa Meneja Mipango WCF, Bw. Patrick Ngwila.
Profesa Katundu akisaini kitabu cha Wageni huku akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Mhe. Abdallah Mtinika (wapili kushoto) na kushuhudiwa na Mwanasheria Mwandamizi WCF, Bw. Deogratius Ngowi.