**************************
Vijana nchini Wanaujiunga na jeshi la kujenga taifa wametakiwa kuondokana na dhana ya kuamini kuwa kujiunga na mafunzo ya (JKT) ni sehemu ya kupata ajira kwani dhamira ya mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uzalendo na kujitegemea.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo, amesema kuwa Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa hasa kwa viongozi wakuu na ndani ya jeshi na kuwataka vijana kuzingatia maadili wanayofundishwa kupitia jeshi kwani wamekuwa na buguza na lugha zisizofaa.
Aidha Jenerali Mabeyo amewataka vijana 2033 walioshiriki kujenga ukuta wa madini huko Merelani mkoani Arusha kwa kujitolea na bado wako katika Makambi au walisharudi nyumbani kuripoti kambi ya Mgulani tarehe 12 mwezi huu kwa ajili ya kuhakikiwa na kukamilisha taratibu za kuandikishwa ndani ya jeshi huku wakiwa na vyeti walichotunukiwa wakati wanamaliza mkataba Wao.
Katika hatua nyengine Jenerali Mabeyo, amesema kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa wa Tanzania na amiri jeshi mkuu amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Meja Jenerali Martini Busungu kuwa Mkuu wa Jeshi la tawi la hakiba Akiba.