Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuwekeza kwenye mchezo wa volleyball ili nao uweze kuongeza ajira kwa vijana na wananchi wote Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya chuo cha Kampala nchini TanzaniaMkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya
pamoja na wachezaji wa timu ya Mafinga mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WACHEZAJI wa mpira wa wavu kutoka katika mikoa mitano ya Tanzania
Bara wamewaomba wadau,taasisi mbalimbali na makampuni kujitokeza kudhamini
mashindano mbalimbali ya mpira wa wavu kwa kuwa umekuwa mmoja ya mchezo ambao
umerudisha mvuto kama ilivyokuwa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa ufundi wa
mashindano ya One Africa volleyball Roben Msigwa alisema kuwa mashindano hayo
yamekuwa yanakuwa siku hadi siku kutokana na mvuto wa mashindano yenyewe.
Alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya
vya wachezaji wa mchezo ambao umekuwa adimu kwenye baadhi ya mikoa hivyo
kupitia mashindano hayo itakuwa chachu ya kukuza mchezo huu kwenye mikoa ya
jirani.
Msigwa alisema kuwa timu ambazo zilishiliki mashindano hayo
ya One Africa ni timu nane ambazo ni Mafinga,Mkwawa,Tumain,Notouris,Best
Six,Combine na Kampala zikiwa zimetoka katika mikoa mitano ambayo ni mkoa wa
Iringa,Mbeya,Ruvuma,Dodoma na Dar es salaam ambazo zilikuwa na wachezaji zaidi
ya mia moja.
Alisema kuwa wamekuwa wakichangishana kuhakiksha wanafanikisha kufanyika kwa mashindano hayo
hivyo wanawaomba wadau,taasisi na makampuni mbalimbali kuwekeza au kudhamini
mchezo wa mpira wa wavu ambao unamashabiki wengi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
ambaye alikuwa mgeni katika uzinduzi wa
mashindano alisema kuwa kunahaja ya viongozi wa michezo wilaya ya Iringa
kuhakikisha wanauzingatia mchezo huo ili uwe unachezwa kwenye viwanja vilivyopo
mkoani Iringa.
Moyo alisema kuwa mchezo huo umekuwa unachezwa kwenye mikoa
ya uwanda wa pwani na baadhi ya mikoa hivyo lazima kuwekeza nguvu na
kuunganisha wadau na makampuni mengine kuwekeza kwenye mchezo huo ambao umekuwa
na mashabiki wengi hivi sasa.
Aliwataka maafisa elimu waliopo katika wilaya ya Iringa
kuweka mikakati ya kufundisha mpira wa wavu ili watoto wanavyokuwa wanakuwa
huku wakijua kuwa kunamchezo mwingine ambao unaitwa volleyball ambao unafaida
pia kwa afya na ajira.
Moyo aliwataka vijana wa wilaya ya Iringa kutumia michezo
kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchukua mikopo inayotolewa na
halmashauri ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana.
Nao baadhi ya wachezaji wa mchezo huo waliwaomba wadau
kujitokeza kuwekeza kwenye mchezo huo wa mpira wa wavu ambao umekuwa mchezo
pendwa kwa jamii ya wanamichezo.
Walisema kuwa mashindano ya One Africa yamekuwa mashindano
ambayo yanawakutanisha watu kutoka mikoa mbalimbali na kuibua upya ya
kupambanania na kuukuza mchezo huo.