Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo(katikati)akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (katikati)akiangalia tumbaku katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU).
………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiwa Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga amewataka wananchi wa mkoa huo na maeneo mengine kuchangamkia kilimo Cha tumbaku kwa kuwa tayari serikali ya CCM imeshughulikia changamoto ya masoko.
Akizungumza katika ziara Wilayani Kahama mkoani humo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema kuwa ameagizwa na Rais Samia Suluhu kuwapa ujumbe Wakulima wa mazao hayo kulima zaidi kwa kuwa kuna Soko la uhakika la mazao hayo.
“Nimezungumza na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mpango wa Wakulima, ameniambia kuwa mpango ni kuzalisha Tani Laki moja au Kilogramu Milioni 100 za mazao haya, maana yake ninyi Wakulima muende kulima maeneo makubwa na Kilimo kikubwa ili uzalishaji uanze kupanda kuanzia sasa”, amesema Chongolo.
Katibu Mkuu amesema Mnunuzi mkubwa wa zao hilo la Tumbaku mkoani Morogoro, alikuwa na changamoto lakini hadi sasa changamoto hizo tayari zimetatuliwa na hivi karibuni Kiwanda hicho kitawashwa kwa ajili ya kufanya uzalishaji, amesema Kiwanda hicho kinahitaji Kilogramu zaidi ya Milioni 30 na zaidi hivyo Wakulima hao wanapaswa kuchangamkia fursa kulima zaidi.
“Tumbaku inauzwa kwa Dola 1.65 ipo hapa inauzwa kwa madaraja ukiitunza vizuri zaidi inaenda hadi daraja la juu inauzwa Shilingi 5000 kwa kilo, sawa na Dola mbili na zaidi, zao la Pamba nalo limeni kwa kiwango kikubwa kwa sababu Soko lipo”, ameeleza