Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ndg. Ramadham Abdala Ali wakati alipowasili katika Ofisi za Mkoa huo leo Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa kamati ya siasa ya Mkoa wa kusini Unguja wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwasalimia viongozi hao katika Ofisi za Mkoa huo leo Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu na Amali, Mhe. Simai Mohamed Said walipokutana leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Mjini Zanzibar. Katikati ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed walipokutana leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani.