Home Biashara TBL YATOA MSAADA WA PRINTER MUHAS NA SHULE ZA ARUSHA

TBL YATOA MSAADA WA PRINTER MUHAS NA SHULE ZA ARUSHA

0

Meneja wa Kiwanda cha  TBL Arusha, Joseph Mwaikasu,akimkabidhi sehemu ya mashine 12 za kisasa (printer),Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro, kwa ajili ya matumizi ya baadhi ya shule zilizopo wilayani humo,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya elimu,makabidhiano yaliyofanyika nje ya ofisi ya Mkuu huyo jijini Arusha.

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi (wa nne kushoto) akimkabidhi   Mkurugenzi Mafunzo   Endelevu na uweledi  wa   Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)   Dkt. Doreen Mloka  (wa pili kushoto) msaada wa mashine  moja ya kuprinti   kati ya 7 zilizotolewa na TBL  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusiadia  huduma  mbalimbali katika kitengo cha  Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell )  nchini.wengine pichani ni wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi akiongea kabla ya kukabidhi msaada wa Printer zilizotokewa na kampuni kwa MUHAS.

**************

Kampuni ya TBL chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBev, katika mwendelezo wake wa kusaidia  masuala ya kijamii, mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa Printa 7 za kisasa kwa kitengo cha  Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell)  kilichopo katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Aidha kampuni hiyo imekabidhi msaada wa Printer 12 mwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro, kwa ajili ya matumizi ya shule zilizopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha sekta ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.

Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutingazi, alisema kuwa kampuni kupitia sera yake ya kujenga Dunia Maridhawa, inaendelea kusaidia changamoto mbalimbali za kijamii hususani katika sekta ya elimu na afya kama ambavyo imetoa msaada wa kusaidia shule na kwenye taasisi ya afya.