Meneja wa Kiwanda cha TBL Arusha, Joseph Mwaikasu,akimkabidhi sehemu ya mashine 12 za kisasa (printer),Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro, kwa ajili ya matumizi ya baadhi ya shule zilizopo wilayani humo,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Serikali katika sekta ya elimu,makabidhiano yaliyofanyika nje ya ofisi ya Mkuu huyo jijini Arusha.
Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi (wa nne kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mafunzo Endelevu na uweledi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Doreen Mloka (wa pili kushoto) msaada wa mashine moja ya kuprinti kati ya 7 zilizotolewa na TBL jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusiadia huduma mbalimbali katika kitengo cha Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell ) nchini.wengine pichani ni wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi akiongea kabla ya kukabidhi msaada wa Printer zilizotokewa na kampuni kwa MUHAS.
**************
Kampuni ya TBL chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBev, katika mwendelezo wake wa kusaidia masuala ya kijamii, mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa Printa 7 za kisasa kwa kitengo cha Afya ya Lishe kwa akina mama wajawazito na ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Aidha kampuni hiyo imekabidhi msaada wa Printer 12 mwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro, kwa ajili ya matumizi ya shule zilizopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha sekta ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.