Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo ameziongoza kamati za Siasa za CCM Wilayani humo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikiwa ni uungaji mkono jitihada za Rais Samia katika kuutangaza Utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
Moyo alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekwishaonesha njia katika kuutangaza utalii hivyo ni muhimu viongozi wa Serikali na vyama vya siasa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada chanya zilizoanzishwa katika utalii
Alisema kuwa amehamasika kuratibu safari ya utalii kwa viongozi wa kamati za siasa za CCM ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia suluhu Hassan chini ya serikali ya awamu ya sita katika kutangaza vivutio hadhimu vya Tanzania kupitia Filam ya Royal Tour
Moyo alisema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kuhamasisha utalii kwa wananchi wengine kwa kuanza kutalii viongozi wenyewe ili wawe mfano kwa vitendo kwa jamii ya kitanzania
Alisema kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini hivyo ni jukumu la kila kiongozi na wananchi kuunga mkono Rais kwenye kampeni hiyo.
Moyo alisema kuwa utalii wa vivutio vilivyopo nchini sio kwa ajili ya wageni kutoka nje ya nchi bali watanzania wote wanatakiwa kwenda kufanya utalii kwenye vivutio hivyo.
Alisema kuwa wameenda kufanya utalii kwenye hifadhi ya pili kwa ubwa nchini na yenye wanyama wa kila aina hivyo anawahamasisha wananchi wengine kwenda kufanya utalii kwenye hifadhi ya Ruaha iliyopo wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa.
Moyo alisema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa ni miongoni mwa hifadhi zinazotajwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo wanyama, ndege aina mbalimbali za miti ya asili , wadudu na vivutio vingine viki ikiwemo vya kipekee
Kwa upande wao Viongozi wa kamati hizo wamepongea hatua ya mkuu wa Wilaya kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa nchini, Wakiweka bayana kuanzia sasa wao ni mabalozi rasmi ya hifadhi hiyo ya taifa
Wenyeviti wa CCM katika wilaya hizi mbili za kichama Costantino Kiwele Kutoka Iringa vijijini na Said Lubeya wa Iringa Mjini walisema kuwa baada ya kufanya utalii kwenye vivutio ya hifadhi ya Ruaha watakuwa mabalozi wa hiyari kuvitangaza vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.
Walisema kuwa hifadhi hiyo imekuwa inamchango mkubwa kwa jamii kutokana na fedha inayoingiza kusaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi.
Waliongeza kuwa hifadhi ya Ruaha imekuwa chachu ya kuutangaza mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujmla hivyo wanaunga mkono alichokifanya Mheshimiwa Rais kwenye Royal Tour ambayo imeanza kuleta neema kwa watanzania.
Naye mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Makala Mapesa aliwahimiza vijana wa kitanzania kuwa na Utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo katika hifadhi mbalimbali hususani hifadhi ya taifa Ruaha
Alisema kuwa ukifika katika hifadhi ya taifa ya Ruaha utafanikiwa kuona vivutio vingi vilivyopo kwenye hifadhi ya hiyo ambayo vitakuanzishia Safari mpya ya maisha yako.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ina ukubwa wa Zaidi kilometa za mraba zipazo 20 elfu ikiwa ni hifadhi ya pili kwa ukubwa ikitakunguliwa na hifadhi ya Nyerere ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa nchini.