WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Muhimbili na shule ya msingi Umoja wa Mataifa kufaidika na Maktaba iliyokarabatiwa na kununuliwa vitabu na wanafunzi waliosoma shule ya Msingi Muhimbili kipindi cha nyuma cha mwaka 1988 ambao amejitolea katika kuboresha elimu katika shule hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi maktaba katika shule ya msingi Muhimbili, Mwenyekiti wa wanafunzi waliosoma katika shule ya msingi Muhimili mwaka 1988, Usia Nkoma amesema kuwa wanafunzi wanaosoma shule ya Muhimbili watumie vizuri Maktaba hiyo kwaajili ya kijiongezea uelewa.
“Maktaba hii itumike na wanafunzi pamoja na waalimu ili kujiongezea uwanda mpana wa kuelewa masomo mnayofundishwa hapa shuleni kwa kuwa mwalimu darasani anakufundisha kwa asilimia 25 na asilimia 75 wanafunzi ndio unatakiwa uelewe ili kukamilisha masomo mliyofundishwa na kutimiza asilimia 100”.
Usia Amesema kuwa Maktaba hiyo iwe kielelezo kwa wanafunzi wengine ambao wataguswa kwaajili ya kuendeleza kuihudumia shule ya Msingi Muhimbili na wao wawe kama walenzi wa shule hiyo kwani wao ndio imewale na mpaka sasa wao bado ni wanafunzi wa shule hiyo.
Nae Mkuu wa shule ya Msingi Mhimbili pamoja na Mkuu wa shule ya Msingi Umoja wa Mataifa wamewashukuru wanafunzi wa shule hiyo wa mwaka 1988 kwa kuona umuhimu waikarabati pamoja na karabati Maktaba katika shule hiyo.
Amesema kuwa wazo la kuikarabati shule ya Msingi Muhimbili lilikuja mara baada ya wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule hiyo mwaka 1988 kuunda kikundi cha pamoja ili kuendeleza taaluma pamoja na shule hiyo.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akizungumza na walimu wastaafu, walimu wa sasa na wanafunzi wa shule hiyo wa sasa na wa waliomaliza mwaka 1988 wakati wa kukabidhi Maktaba iliyotolewa na wanafunzi wa Mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili.
Mwenyekiti wa Wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili, Usia Nkoma akizungumza na wanafunzi wa sasa na wa mwaka 1988 pamoja na walimu wastaafu na wasasa wa shule hiyo wakati wa kukabidhi Maktaba katika shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mtaifa, Woindumi Siyao akiwashukuru wanafunzi wa shule ya Msingi Muhimbili wa mwaka 1988 katika shule hiyo kwa kuikumbuka na kujitolea kuikarabati na kuifanya iwe na Maktaba.
Kiongozi wa Dini ambaye pia ni mwanafunzi aliyesoma shule ya Msingi Muhimbili akiomba ili shughuli ya kukabidhi Maktaba katika shule hiyo iende vizuri.
Baadhi ya walimu wa sasa wa shule ya msingi Muhimbili.
Baadhi ya walimu wa Staafu wa shule ya Msinmgi Muhimbili wakiwa moja ya wageni walioalikwa na wanafunzi waliosoma katika shule ya Msingi Muhimbili mwak 1988 jijini Dar es Salaam.
Katibu na Muweka hazina wa wanafunzi waliomaliza shule ya Msingi mwaka 1988.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muhimbili na wahitimu watarajiwa katika shule hiyo.
Meza Kuu katika kukabidhi ukarabati wa Maktaba katika shule ya Msingi Muhimbili leo jijni Dar es Salaam.
Badhi ya walimu wastaafu waliokuwa wakifundisha shule ya Msingi Muhimbili wakizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo leo wakati wa kukabidhi Maktaba iliyotolewa na wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akikata utepe kuzindua Maktaba iliyotolewa na wanafunz waliomaliza mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbiliwakishirikiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mtaifa, Woindumi Siyao, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili, Usia Nkoma na Mkuu wa shule ya Msingi Muhimbili, Jovita Mushi.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala, Abirah Mchia (Mwakilishi wa Mkuruge nzi Manispaa ya Ilala) akifungua kitabu cha Satadi za kazi mbele ya walimu wastaafu, walimu wa sasa na wanafunzi wa shule hiyo wa sasa na wa waliomaliza mwaka 1988 wakati wa kukabidhi Maktaba hiyo kwa Mkuu wa shule ya Msingi Muhimbili na Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyotolewa na wanafunzi wa Mwaka 1988 katika shule ya Msingi Muhimbili.
Maktaba katika shule ya Msingi Muhimbili iliyotolewa na akukarabatiwa na wanafunzi wa shule hiyo wa mwaka 1988.