Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa kushirikiana na Taasisi ya walemavu wa Uti wa mgongo KASI imetoa misadaa mbalimbali kwa walemavu wenye matatizo ya Uti wa Mgongo walioko katika wilaya ya Arumeru
Dc Muro ambae ameamua kuonyesha juhudi binafsi katika kuwasaidia watu wenye ulemavu amesema wametoa misaada ya kuanza maisha ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu ili waweze kumudu maisha hatua itakayowasaidia kuwaondoa katika kundi la utegemezi katika familia jambo linalochangia watu kuwanyanyapaa
Misaada iliyotolewa ni vifaa vya kuanzisha biashara ya vifaa vya ujenzi, maji kwa ajili ya mradi wa kuuza maji ya jumla , vifaa vya majumbani zikiwemo chupa za chai , hotpot, mamia ya kuku wa kienyeji kwa ajili ya bishara ya mifugo, mbuzi pamoja na bidhaa mbalimbali
Wakizungumza mara baada ya Dc Muro kukabidhi misaada hiyo, kiongozi wa jumuiya ya watu wenye ulemavu wa uti wa mgongo kwa mikoa ya kilimanjaro na Arusha KASI Ndugu Deogratiua Chami ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu hatua inayowasaidia kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto walizonazo ambapi amesema wao kama KASI wanapambana kuwafikia walemavu wengi zaidi katika ukanda wa kaskazini
Kwa upande wao viongozi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kichama ya Meru wakiongozwa na katibu mwenezi Comrade Joshua Hungura wamesema jitihada zinaonyeshwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru katika kuyafikia makundi mbalimbali yenye mahitaji maalum ni kielelezo tosha cha utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika kuwahudumia watu wenye ulemavu