Pipipiki za matari matatu maarufu kama bajaji zilizokuwa zimefunga barabara ya Mjini – Masika Manispaa ya Morogoro.
Pipipiki ya matari matatu maarufu kama bajaji ikipandishwa kwenye gari la manispaa baada ya kukamatwa katika operesheni ya kuziondoa pikipiki hizo zilizokuwa zimefunga barabra.
Baadhi ya Madereva wa Pipipiki ya matari matatu maarufu kama bajaji wakiwa katika mgomo.
……………………………………………………
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
MADEREVA wa Pipipiki ya matari matatu maarufu kama bajaji ambao wanatoa huduma ya usafiri manispaa ya Morogoro wamefunga barabara ya Mjini – Masika kwa saa kadhaa wakishinikiza uongozi wa mansipaa ya Morogoro na kikosi cha usalama barabarani kuwaaacha waendele na zoezi la kupaki pikipiki hizo katika eneo la Islamu na Luna hali iliyolizazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuwaondoa kwa nguvu .
Akizungumza mara baada ya operasion hiyo mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Michael Deleli amesema kuwa wamelazimika kuwaondoa ili kupunguza msongamano wa watu katika barabara hiyo ambao ulikuwa unasababaishwa na kuengesha bajaji bila ya utaratibu kama anavyoleza
Mhandisi Godwini Mpinzile ni mratibu Wakala wa barabara vijiji na mjini TARURA amesema madereva hao walishapewa maelekezo sehemu za kwenda kuegesha bajajai zao lakini wamekuwa wakikaidi kufuata malelekezo hayo huku afisa mfawidhi mamlaka ya Uthibiti wa usafiri wa ardhini LATRA Bw. Adrew Mlacha ametolea ufafanuzi suala la leseni za bajiji na utaratibu wa kufuata wakati wa kutoa huduma ya usafiri.
Nao baadhi ya madereva wa bajaji akiwemo Bw. mfaume Yasini na Bw. Daudi Zungu wamesema hawakati kuondoka katika eneo hilo lakini wameomba kuboreshewa mazingira kama madereva wa magari kwani nao wanalipa ushuhuru kama vyombo vingine vya usafiri.
Hayo Yamejiri Baada Ya Halamshauri Ya Manispaa Ya Morogoro Kutoa Maelekezo Kwa Waendesha Babaji Kurejea Katika Vituo Vilivyopangwa Kuanzia Tarehe 5 Mwezi 9 Mwaka 2019.