Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakati wakizungumza na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel katika mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel mara baada ya mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wakizungumza na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel katika mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakisindikizwa na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Ushirikiano wa mambo ya nje nchini Israel Ndg Yuval Fuchs mara baada ya mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.

 

Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel

 

Waziri wa Kilimo wa

Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 5 Septemba 2019 amekutana na

kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel.

 

Katika mkutano huo wa

kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa

namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, Waziri wa Kilimo

amewasilisha mambo mbalimbali kuhusu sekta ya kilimo ikiwemo ufuatiliaji wa

utekelezaji wake.

 

Mhe Hasunga

ameishukuru serikali ya Israel kwa kukubali ombi la Rais wa Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoshiriki

mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka 45

ambapo imefikia idadi ya wanafunzi 100.

 

Katika kikao hicho Waziri

Hasunga amewakumbusha Mabalozi hao sita kuhusu ombi la Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongezwa idadi ya

wananfunzi kufikia idadi ya wanafunzi 300.

 

Mhe Hasunga amesema

kuwa Balozi huyo amepongeza kwa dhati na kuunga mkono juhudi za serikali ya

Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwani ni serikali ya

vitendo na uwajibikaji hivyo wapo tayari kuhakikisha kuwa ushirikiano

unaboreshwa baina ya nchi hizo mbili.

 

Kikao hicho pia

kimejadili kwa kina namna ya kuboresha zaidi mahusiano baina ya nchi ya

Tanzania na Israel hususani katika kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za utafiti,

uongezaji thamani wa mazao, na namna ya kuongeza ukubwa wa mashamba na kilimo

tija.

 

Pia, Mhe Hasunga

amewasilisha ombi la kupata kampuni mbalimbali za nchini Israel ili kuzuru

Tanzania na kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji.

 

“Tukipata kampuni za

kuisaidia Tanzania kwenye maswala ya kilimo cha umwagiliaji tutakuwa na fursa

ya kubadili kilimo chetu kutoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua na hatimaye

kuingia katika kilimo cha umwagiliaji” Alisisitiza Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

 

 

Serikali ya Israel

imekubali kufikiria kuongeza idadi ya vijana kutoka Tanzania wanaozuru Israel

kwa ajili ya kujifunza ambapo pia wataongeza uwezekano wa wataalamu mbalimbali

wakiwemo maafisa ugani nchini Tanzania kuzuru Israel kwa ajili ya kujengewa

uwezo katika utendaji.

 

Kwa upande wake Naibu

Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Ushirikiano wa mambo ya nje nchini Israel

Ndg Yuval Fuchs amesema kuwa serikali ya Israel imeridhia maombi ya Waziri wa

Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga na kusema kuwa Israel ipo tayari

kushirikiana na Tanzania ili kuboresha sekta ya kilimo kutoka kwenye kilimo cha

kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara

 

Vilevile amesema kuwa

atazishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini Tanzania kwa ushirikiano mzuri

na serikali kwani Tanzania kuna ardhi nzuri yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.

 

Kadhalika amempongeza

Waziri Hasunga kwa kutembelea nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo

amesema kuwa kumekuwa na kikao muhimu kilichojadili namna ya kuboresha kilimo

nchini Tanzania.

 

Kadhalika,

Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima amesema kuwa kikao cha

Waziri wa Kilimo ni muendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo nchini Israel ambapo

ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa taswira ya kutafakari kwa pamoja kuona namna

mafunzo hayo yanavyowasaidia vijana wa kitanzania.

 

Amesema

Waziri Hasunga amekutana na ujumbe wa mabalozi 6 pamoja na wasaidizi wake

wanaohusika na maswala ya Afrika Mashariki, kikao hicho kimetoa heshima kubwa

kwa serikali ya Tanzania ambapo vijana 100 watapokelewa nchini Israel na waziri

Hasunga leo tarehe 5 Septemba 2019.

 

Naye Mkurugenzi

Mtendaji wa Taasisi ya agrostudies Ndg Yaron Tamir amesema kuwa wanafunzi walioshiriki

mafunzo hayo kutoka Tanzania wametoa ushirikiano mzuri hivyo mafunzo hayo waliyoyapata

wanapaswa kuyaendeleza ili kuboresha kilimo nchini Tanzania.