……………………..
Story na farida said,morogoro
KATIKA kupambana na vitendo vya ya ukatili wa kijinsia Chama cha
SCOUT Taifa kimeanda mkakati wa kukabiliana na matukio hayo kwa
kuandaa midahalo mbalimbali itakayowakutanisha vijana wa chama
hicho kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro ili kufahamu adhari za
ukatili na namna ya utoaji wa taarifa kwa waathirika wa janga hilo.
Wakizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya SCOUT mjini
Morogoro mwenyekiti wa vijana wa chama cha SCOUT Taifa Bw.
Yasin Makaraba na kamshina wa Vijana wa chama hicho Bw.
Abukari Mtitu wamesema kazi moja wapo ya chama hicho ni kulea
vijana katika maadili bora hivyo kuwepo kwa matukio ya ukatili
wanawajibu wa kupambana kwa dhati ili kuelimisha jamii athari za
matukio hayo hivyo wanatarajia kuandaa mkakati utakao saidia
kupambana na changamoto hiyo.
Kwa upande wake afisa elimu ya watu wazima Mkoa wa morogoro Bi.
Rodah Sheba amesema kuongezeka kwa matukio ya ukatili
unachangia watoto wa mitaani hivyo progamu hiyo imetajwa kuwa
mwarobaini wa changamoto hiyo.
Mashindano hayo yameanza septemba Tatu mwaka huu na
yanatarajiwa kukamilika septemba saba mwaka huu huku lengo likiwa
ni kupata washindi watakaoliwakilisha taifa katika mashindano ya
SCOUT Afrika yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu nchini
Sudani ya kusini na kwamba pamoja na mambo mengine washiriki zaidi
ya 50 watapata fusra ya kuonesha vipaji balimbali ya ubunifu.