Bw. Julius Nguhulla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kulia ni Joel Uronu Katibu wa Chama cha Mawakala wa Meli (TASAA).
……………………………………………………
MBOBEZI wa Kimataifa katika shughuli za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli ambaye pia ni Mtanzania pekee kati ya wawili waliopo Tanzania wenye ubobezi wa aina yake aliyepo kwenye bodi ya watalaamu wa biashara ya usafirishaji wa mzigo kwa njia ya meli Duniani( ICS,) Julius Nguhulla(FICS) amesema ataendelea kumshauri Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kuhusu sekta ya meli nchini kwa maslahi ya Watanzania wote.
Nguhulla amesema Juni 3 mwaka huu wa 2019 kwa nia njema alimuandikia barua ya kumpongeza Rais wetu kwa kazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwani pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Meli Tanzania(TASAC)ambapo pia aliomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.
Hata hivyo alitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli na bandari.
Nguhulla ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Salaam wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo amesisitiza amewahi kumshauri Rais Magufuli kuhusu sekta ya meli kupitia barua yake hiyo aliyomuandikia .
“Tangu mwaka 2016 nimekuwa nikijishughulisha na kazi za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli.Mimi ni miongoni mwa watu Duniani waliokwenye Bodi ya wataalumu wa biashara ya usafiri wa mizigo kwa njia ya meli yaani shipping.
“Kutokana na ubobezi wangu katika usafiri wa mizigo kwa njia ya meli nimekuwa nikishiriki kutoa ushauri wa kitaalamu wa mambo ya meli na bandari ndani na nje ya Tanzania.Kupitia ubobezi wangu tarehe 03.06.2019 niliandika barua kumpongeza Rais wetu kwakazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa TASAC.
“Kadhalika , nilimwomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.
“Hata hivyo nilitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli,”alisisitiza Nguhulla.
Alifafanua zaidi kwa kutumia ubobezi wake katika sekta ya bandari na meli hatasita kutoa ushauri kwa wakuu wa nchi na hasa Rais Magufuli ambaye amekuwa mzalendo kwa nchi yake,hivyo kuna kila sababu za Watanzania wa kada mbalimbali akiwemo yeye kumshauri kwa kufuata taratibu za nchi bila kuvunja sheria.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumuandikia barua Rais, amesikitishwa na namna ambavyo mmoja ya wanaharakati kumtusi na kutoa maneno ya kejeli dhidi yake.
“Agosti 26, mwaka 2019 mtu mmoja alinitukana kwa kutumia moja ya televisheni nchini na kusema mimi nilimwandikia barua kumshauri Rais kuhusu waraka unaoitwa delivery order na tozo zake.Mtu huyo alinichafua na kunitukana kwa kutaja jina langu kwa kudai kwamba kwa uamuzi huo mimi nilioufanya mimi ni mjinga na mpuuzi kabisa na sijui chochote,.
“Waandishi wa habari ni kweli nilimwandikia barua Rais nikimshauri kuhusu mada kama nilivyotaja hapo juu nikiwa na haki ya kumshauri Rais wangu kwa lengo la maendeleo ya Taifa langu lakini, hata hivyo nimedhalilishwa kwa kutukanwa kama nilivyoainisha hapo juu huku nikitajwa Jina langu,”alisema.
Alifafanua kuwa ameambiwa amemdanganya Rais wetu kuwa shipping ni taaluma yake na kwamba hajawahi kufanya kazi ya aina hiyo popote.Hivyo alisema kwa sababu upotoshaji na udhalilishaji huu ulifanywa kwenye chombo cha habari umma wa watanzania ukasikia na yeye ameona atoe sikitiko lake la kutukanwa mbele ya Umma wa Watanzania.
Pia alisema amejitokeza hadharani kukanusha mbele ya umma wa watanzania kwamba yeye hakumdanganya Rais kwamba shipping ni taaluma yake,hivyo aliamua kutoa ufafanuzi hatua kwa hatua kuhusu shughuli ambazo amezifanya.
Nguhullla amewaambia waandishi wa habari kuwa anayo shahada ya heshima kutoka nchini Uingereza kuhusu mambo ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli yaani Shipping baada ya kusomea kwa miaka mitano na kuingia kwenye bodi ya wataalamu wa shiping wa dunia ambapo chao cha juu cha kitaalam kwenye masuala ya biashara ya meli ni cha mtu anayeitwa FICS ambapo kwa Tanzania imefanikiwa kumtoa mtu mmoja ambaye ni yeye kati ya watu 2000 duniani.
Pia anayo Masters ya Biashara ya meli yaani MBA in shipping aliyoisomea Cyprus na sasa anaendelea na utafiti( Global Business University).
Alisema anao uzoefu wa miaka 15 ya kazi za meli( uwakala wa meli) na amewahi kufanya kazi na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC wa sasa kwa muda wa miaka mitatu akiwa mwajiri wake na kuongeza kila mwaka huwa anaenda nje ya Tanzania kwa ajili ya mikutano ya shipping pamoja na kufundisha.
“Sisemi haya kujisifu ila namshukuru Mungu maana yeye peke yake ndio wakusifiwa. Kadhalika , Serikali yangu ya Tanzania imekuwa ikinihusisha sana na shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya kuelimisha kuhusu shipping na mengineyo. Ipo siku nilitoa somo nikiwa na CEO wa TICTS tulipoalikwa na serikali kueleza umuhimu wa Teknolojia katika Port Operations. Serikali imewahi kuniomba kuwafanyia interview wakurugenzi waliokuwa wanataka kuajiriwa kwenye ofisi ya Serikali inayohusika na shipping.
“Nimewahi kuombwa na TRA kufanya mafunzo kwa siku mbili katika kitengo cha enforcement kuhusu Bill of Lading. Pia Januari mwaka 2018 nilitoa Presentation Tanzania ikijumuisha watu wa Serikali , na wamiliki wa meli wa mataifa mbalimbali , idadi ya watu ikiwa ni 200 kuhusu matumizi ya bill of leading, manifest na mengine mengi,”alisema.
Alisisitiza bila uzoefu wake na taaluma aliyonayo Serikali yake isingempa heshima kama hiyo ambayo ameianisha na kumuomba mtu asitumie cheo chake ambacho amepewa na Mungu kuwatumikia watanzania kwa kutukana watu na taaluma zao.
“Namheshimu sana mtu huyu na nitaendelea kumheshimu na nina msamehe maana umri wake kwangu ni kama baba yangu. Na haya niliyosema si kwamba namshambulia ila naeleza ili Umma ufahamu kuhusu mimi na kupuuza upotoshaji uliofanywa dhidi yangu na heshima ya taaluma yan,”alisema Nguhulla.
Alisisitiza watanzania wanayofursa sawa ya kumshauri Rais pasipo kuvunja sheria na kwamba kama wameamua kuzungumzia maslahi yaTaifa ,basi waendelee na mtazamo huo huo badala ya kuhamia katika maslahi binafsi.