Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amepokea Mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Mirathi na Sheria ya Ndoa yaliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mhe. Makonda amewasilisha mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya hizo kwa Mhe. Dkt Mahiga ili zifanyiwe marekebisho na kuendana na wakati na zitoe haki kwa wanawake nchini pindi Mume anapofariki na hivyo kuwaondolea mateso na manyanyaso Wajane nchini.
Akizungumza baada ya kupokea mapendekezo hayo Mhe. Mahiga amemuahidi Mhe. Mkuu wa Mkoa ambaye aliambatana na viongozi wa Chama cha Wajane Tanzania kuwa Wizara itayapitia mapendekezo yao na kuyafanyia kazi stahiki.
“Niwashukuru kwa kazi hii kubwa mliofanya ambayo Mhe. Mkuu wa Mkoa umenikabidhi leo hii, hii ni ishara ya kazi kubwa na nzuri unayoifanya kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam, nikuahidi wewe na timu yako kwamba mimi na timu ya wataalamu wangu tutayapitia mapendekezo yenu na kuyafanyia kazi ili tuweze kwenda na wakati na kutoa haki kwa wananchi wetu,” alisema Mhe. Waziri
Amesema Wizara ya Katiba na Sheria itahakikisha inalifanyia kazi suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa utafiti huo umefanywa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao una uwakilishi wa watu kutoka mikoa yote nchini na kuongeza kuwa haki nyingi za wanawake zimekuwa zinadaiwa lakini suala la mirathi ni kama limesahauliwa.
Awali akikabidhi taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema Sheria ya Mirathi ya Mwaka 1865 , Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini ya Mwaka 1963 zimeonekana kuwa na Mapungufu makubwa na zimepitwa na wakati na kutokana na hali hiyo zinawakandamiza wanawake na kuwanyanyasa.
Ametaja vipengele wanavyopendekeza kufanyiwa marekebisho kuwa ni pamoja na kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemuutafiti kutoondolewa kwenye nyumba, Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja na haki ya mtoto wa nje ya Ndoa, Mjane kutoondolewa kwenye nyumba.
Vifungu vingine ambavyo Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kile kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo.
Amesema utafiti waliMjane kutoondolewa na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 aliokutana nao mwezi April ambapo alipokea Kero na Malalamiko mbalimbali kutoka kwa Wajane waliohudhuria kongamano hilo na kuamua kuunda kamati iliyoshirikisha Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia ambao waliopitia malalamiko hayo na kuja na mapendekezo hayo.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania Bi Rose Sarwat ameishukuru Wizara kwa kukubali kupokea mapendekezo hayo ili kuyaangalia na kuja na marekebisho ambayo yatawafanya wajane nchini kuishi kwa amani na upendo baada ya kufiwa na waume zao.