Vijana wa Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Misungwi wakimvisha skafu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli alipokwenda kwenye ziara ya kikazi katika kata za Mbarika na Misasi jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na Makatibu wa Kata na Matawi wa Chama (hawapo pichani) wa kata za Mbarika na Misasi kwenye tarafa ya Misiasi wilayani Misungwi.Wa pili kutoka kulia ni Katibu wa CCM Misungwi, Latifa Malimi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli akisitiza jambo kwa makatibu wa matawi na kata za Misiasi na Mbarika wilayani Misungwi jana.
Katibu wa CCM Wilaya ya Misungwi, Latifa Malimi (kulia) akipokea bendera 550 kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (kushoto), ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally, aliyoyatoa wakati wa ziara yake mapema mwezi Agosti mwaka huu.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.
Picha na Baltazar Mashaka