ABDALLH MANGALA MWENYEKITI WA AASISI YA JICHO LA MAMA SAMIA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI.
SULEIMAN MANGALA MAKAMU MWENYEKITI WA TAASISI YA JICHO LA MAMA SAMIA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MKITANO HUO..
Taasisi ya Jicho la Mama Samia ilianzishwa Julai 2021 na Watanzania wazalendo wenye mapenzi mema na Nchi kwa lengo la kufanya utafiti na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa Rais hasa akiwa ameingia katika Historia ya kuwa Mwanamke wa Kwanza hapa Nchini Tanzania kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwa kudra za Mwenyezi Mungu amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati Dk. John Pombe Magufuli jambo ambalo halikuwa limetegemewa na Watanzania walio wengi.
Taasisi ya Jicho la Mama Samia itakuwa na jukumu la Kufanya Utafiti na kufuatilia mambo yanayofanywa na Mama Huyu ambaye Mwanamke na ni Kiongozi shupavu kwa yale mazuri anayofanya Vizuri tutayaainisha na kueleza kuwa unafanya Vizuri boresha jambo hili na lile kwa yale yenye Changamoto tutamueleza Changamoto na kupendekeza utaratibu bora wa Utatuzi wa Changamoto hizo.
Inaungana pia na Watanzania walio wengi waliompongeza Rais wa awamu ya Sita Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha Mwaka mmoja akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ameweza kusimamia utekelezaji wa Ilani wa CCM kwa ukamilifu mkubwa pamoja na ile miradi Mikubwa ya Kimkakati
Miradi hiyo ni kama kuhamia Makao Makuu Dodoma na kuimarisha miundo mbinu kazi inayoendelea, Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kazi inaendelea kwa kasi kubwa, Ujenzi wa Reli ya Kisasa kazi inaendelea kwa kasi kubwa, Miradi ya Maji vijijini na Mijini Watanzania ni mashuhuda jinsi Mama anavyopambana kuhakikisha kila Mtanzania anapata Maji safi na Salama.
Kuhusu miundo mbinu tunashuhudia barabara za Mijini na Vijijini zikitengenezwa kwa kasi kubwa. Lakini kikubwa kilichowashutua Watanzania nio ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa Nchi nzima na kuanza kutatua kero sugu ya muda mrefu iliyosababisha watoto wetu wakati mwingine kuingia Kidato cha Kwanza kwa awamu mbili au Tatu
Katika hatua nyingine Rais Mama Samia amerudisha mahusiano ya Kimataifa ambayo yalianza kuzorota, hii imeweza kufungua Misaada na Mikopo kwa ajili ya Kuharakisha maendeleo ya Nchi, na pia imewezesha wawekezaji wengi kurudisha matumaini ya kuja kuwekeza na wote ni mashuhuda wa matokeo ya Mkutano wa Dubai Expo ambapo wawekezaji wengi waliahidi kuja kuwekeza Tanznaia
Moja ya mambo muhimu ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameyaangazia pia ni suala zima la uhuru wa vyombo vya habari Wote ni mashuhuda kuwa kulikuwa na Kilio kikubwa cha uhuru wa habari.
Kulikuwa na malalamiko makubwa uhuru wa Vyombo vya habari umeminywa sana na kulikuwa na hofu ya watu kuzungumza. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani aliweza kukutana na wahariri wa Vyombo vya Habari na Kuzungumza nao na kuahidi kuyafanyia kazi mambo yote yaliyoibuliwa.
Tumeshuhudia uhuru wa Vyombo vya Habari ukiongezeka, vyombo vilivyofungiwa vimeruhusiwa kuendelea na kazi. Gharama za kusajili vyombo vya mitandao zimepungua na Hofu ya wananchi kuzungumza na kutoa maoni yao imeondoka kabisa
kwa upande wa suala zima la Demokrasia ya vyama vya siasa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya ndani nan je ya Nchi kuhusu kuporomoka kwa Demokrasia Nchini kitu kilichopelekea kuwa na makelele mengi na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa kutokana na matamko mbalimbali kutoka kwa wana Siasa na wana harakati.
Tunamshukuru na Kumpongeza Sana Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kuridhia Baraza la Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili kuitishwa kwa Mkutano wa Wadau ili waweze kujadili kwa uhuru mustakabali wa Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania.
Lakini Rais alichukua hatua ya Kwenda kufungua Mkutano ule na kutoa nasaha na Maelekezo yake lakini pia katika utamaduni wa Kudumisha Muungano Rais wa Zanzibar alikuja kufunga pia kutoa nasaha na maelekezo yake.
Mambo mengi yalizungumzwa na kupelekea kuundwa kwa kikosi kazi ambacho kilipewa jukumu la kuchakata maoni ya wadau na kutoa mapendekezo.
Kikosi kazi kimewasilisha taarifa ya awali kwa Rais ikielekeza jinsi itavyafanya kazi ya kuyafanyia kazi maoni ya wadau kwa kuzidi kupata maoni ya wadau mbalimbali tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuruhusu mjadala wa hatma ya Demokrasia ya Mfumo wa Vyama vingi hapa Tanzania.
Haya ni baadhi ya Mambo machache kati ya mengi ambayo ameyafanyia Rais katika kipindi cha mwaka mmoja wa Uongozi wake Tunaungana na Watanzania wote kumshukuru na Kumpongeza sana