Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akiwa ameshika mkuki
huku amevaa mavazi maalum baada ya kusimikwa kuwa Chifu wa Kijiji
cha Ihalula, kutoka kwa mmoja wa wazee wa kimila( aliyesimama kulia),
baada kuwasha umeme katika kijiji hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( wa pili kulia) akitoa maelekezo
baada ya kutembelea chumba kujifungulia akina mama wajawazito katika
Kituo cha Afya cha Ihalula, katika halmashauri ya wilaya ya Njombe,
mkoani njombe,baada ya kuwasha umeme katika zahanati hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto) akigana na Mbunge
wa Wanging’ombe, Gerson LWENGE( kulia) baada ya kuwasha umeme
katika Kijiji cha Itombololo, wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( katikati) akikata utepe kushiria
kuwasha umeme katika moja ya shule za msingi katika Kijiji cha Saja,
wilayani ya Wanging’ombe mkoani Njombe.
***************
Na Zuena Msuya, Njombe
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amesema zoezi la mwakijiji
yeyote kuunganishiwa umeme ni lazima siyo hiari kwa kuwa kila mtanzania
hasa walio vijijini wanamudu gharama ya kuunganishiwa umeme kutokana
na kiwango cha gharama kilichopangwa na serikali.
Dkt.Kalemani alisema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme vijijini(REA) ili uweze
kuwafikia wananchi wote walioko vijijini ambao wanatakiwa kuchangia kiasi
kidogo cha fedha ili kuunganishwa na huduma hiyo.
Dkt.Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika vijijini vinne
ambavyo ni Ihalula, Itombololo, Itowo na Saja vilivyopo katika Halmashauri
ya Wilaya Njombe na Wanging’ombe mkoani Njombe, Septemba 2,2019.
Kwa mujibu wa Dkt.Kalemani, Serikali iliangalia hali ya uchumi kwa
wananchi wake wote hasa wanaoishi Vijijini na kujiridhisha kuwa kila
mlengwa anauwezo kwa kuchangia shilingi 27,000/= ikiwa ni gharama
nafuu ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa gharama zingine za kutekeleza
mradi huo zinalipwa na serikali.
Alifafanua kuwa zoezi kuunganisha umeme kwa kila nyumba ya mwanakijiji
anaeishi kijijini ni lazima kwa sababu Mradi wa Usambaji Umeme Vijijini(
REA) unaunganisha nyumba za aina zote na maeneo yote ya vijijini bila
kujali itikadi za Kisiasa, Imani za Dini, wala Kabila.
Aliendelea kusisitiza kuwa, hapo baadaye serikali itafanya zoezi la kukagua
nyumba moja baada ya nyingine zilizopo vijijini kufuatilia zoezi la
uunganishwaji wa umeme kwa wanavijiji, na endapo watabaini kuwa
mwakijiji ameshindwa kuunganisha huduma hiyo bila sababu ya msingi,
basi itamlazimu kuuza mifugo au mazao ili kupata shilingi 27,000/= ikiwa ni
gharama ya kunganisha umeme kwa lazima.
“Zoezi la kuweka umeme katika kila nyumba vijijini ni lazima siyo hiari
kama mnavyodhani, serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza mradi wa (
REA),pia ni nia ya kuwasogezea huduma bora na za msingi kwa
maendeleo ya wananchi wake, ambao na wao watachangia gharama
ndogo: Sasa usipoweka umeme tutakuja kuuza chochote unachozalisha
nyumbani kwako tukulipie huduma hii”. Alisema Dkt.Kalemani.