
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amesema Bunge lina mpango wa kuacha kutumia mfumo wa sasa wa makaratasi Bungeni, kwa ajili ya kuwapa Wabunge nyaraka mbalimbali, watakachofanya sasa ni kuhamia katika mfumo wa Digitali, kwa kuwawekea kupitia kwenye simu zao.
Amewataka wabunge kuthibitisha namba zao za simu wanazozitumia katika mtandao wa WhatsApp na email kwa ajili ya kuanza kupatiwa orodha ya shughuli za Bunge kwa siku husika kwa njia ya mtandao.