Dondoo za mkutano wa jana Baina ya Matawi na Mwenyekiti wa klabu Mshindo Msolla
Mkutano ulikua na lengo moja kuhamasisha amani na umoja ndani ya Yanga kuelekea mechi na Zesco pamoja na mechi 37 za ligi kuu zilizobaki
Matawi yasaidiane pamoja na klabu kuhakikisha Yanga inashinda mechi zake zote zilizobaki za ligi kuu pamoja na mechi ya Kimataifa
Katika kuleta umoja wa klabu tuondoe makundi makundi yote yaliyokuwepo Wakati wa uchaguzi na Sasa Yanga iwe moja atakayechochea makundi kupelekwa Kamati ya Nidhamu kushugulikiwa
Matawi yafanye chaguzi kufikia December na katika kuhakikisha Hilo litasimamiwa Mwenyekiti yupo mbioni kuunda Kamati ya Matawi na wanachama itakayokua inasimamia Masuala ya Matawi na wanachama kwa ujumla.
-Kwa muda wa miezi minne Kamati mpya ya Utendaji imekwisha ingia mikataba zaidi ya minne kuhakikisha Yanga inakua vyema kiuchumi
-Jengo la klabu Yetu Sasa ukarabati utaanza muda sio mrefu na utafanywa na Kampuni ya GSM kwa kua moja ya masharti katika tender ya jezi iwaliyopewa limo pia sharti la kukarabati Jengo ili Sasa Tupunguze matumizi ya kukaa hotelini,ukarabati utahusisha pia sehemu ya mazoezi ya viungo Gym pamoja na bwawa la kuogelea lililopo katika Jengo letu.
Mpaka Sasa Yanga Ina mkataba na Sportpesa ambao mwaka huu watatoa Bilioni Moja na milioni 94,Uongozi umefanikiwa kupataa mikataba na Taifa Gas toka kwa Rostam ambao watato milioni 300 lakini pia ushirikiano na Mh Rostam bado upo ndie aliyetoa milioni 60 kuvunja mkataba wa Kindoki na pesa za kumleta Molinga Yanga,Mkataba na GSM wa Kwanza ni ule wa jezi ambao klabu unapata TSH 1300 kwa kila jezi itakayouzwa na lengo ni kuhakikisha jezi milioni 1 zinauzwa ili klabu ipate Bilioni Moja na milioni 300 ,pia mkataba unahusisha ukarabati wa Jengo la Yanga,Mkataba wa pili na GSM unahusisha magodoro ya GSM mkataba huu una thamani ya milioni 150, Klabu ipo mbioni kuongeza mdhamini mwingine toka Kampuni ya Vinywaji atakayetoa pesa Kama ilivyo Sportpesa na pia kukarabati pitch ya uwanja wa Kaunda uwe wa kisasa kutumika katika mazoezi ndio maana zoezi la kuweka kifusi linaendelea kwa kasi.
Si kweli kwamba Mwl Zahera amepewa siku Tatu Bali juzi Kulikua na kikao cha Kamati ya Utendaji na kocha aliitwa atambulishwe rasmi kwa wajumbe na pia ashauri mikakati ya kuelekea mechi na Zesco na kiujumla Uongozi una imani na kocha na wanaushirikiano mzuri hivyo habari kua amepewa mechi tatu tuzipuuze.
Kuhusu sectretaliet tayari mchakato wa kuwapata Katibu na wakurugenzi wa idara mbalimbali Kama Fedha ,Masoko,Ufundi na Mashindano umeshakamilika na wiki hii watapewa ofa ya mikataba tayari kwa kuanza kazi
Timu itaelekea Mwanza kwa maandalizi ya mechi na Zesco itaondoka Tarehe 4 Mpaka tarehe 11 Itakua Mwanza ,ikiwa Mwanza kutakua na Kubwa Kuliko tamasha la kuichangia Yanga lililoandaliwa na wanayanga wenyewe wa Mwanza,wana Mwanza wamelipia kila kitu kuhusu safari hiyo hivyo klabu haitahusika na gharama yeyote na itafaidika katika mechi 2 za kirafiki kwa kupata 85% ya gate collection.
Gazeti la Yanga liko mbioni na litalejea mda sio mrefu
Mwisho wanayanga wote tusameheane wale waliokua nje ya Timu na sasa wamerudi Ni juhudi za Mwenyekiti kuhakikisha Yanga yote tunakua wamoja hivyo tusijenge visasi tunapowaona tushirikiane nao kuhakikisha Yanga inakua moja.
Kila mwanachama asiache kuhudhuria mechi yetu na Zesco.
Katibu Tawi VIVA