Home Mchanganyiko WANACHAMA CHAMA CHA MADAKTARI WA KIKRISTO TANZANIA WAASWA  KUFUATA TARATIBU ZA MATUMIZI...

WANACHAMA CHAMA CHA MADAKTARI WA KIKRISTO TANZANIA WAASWA  KUFUATA TARATIBU ZA MATUMIZI NA MANUNUZI YA FEDHA KWA UWAZI

0

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkurugenzi  mtendaji wa Taasisi ya kidini ya Christian Social Services Comission[CSSC]inayosimamia  sekta Afya na Elimu kwa Baraza la Maaskofu Makatoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania,Peter Maduki  amewaasa washiriki na wanachama cha madaktari wa Kikristo Tanzania,Tanzania Christian Medical Association[TCMA] amewaasa wanachama wa hicho kufuata taratibu za Matumizi na Manunuzi ya Fedha kwa Uwazi bila Ubadhilifu kama ilivyoelekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali [C.A.G.

Mkurugenzi huyo wa CSSC ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika mkutano wa chama cha Madaktari wa kikristo Tanzania [TCMA] ambapo amesema manunuzi na matumizi ya fedha yanatakiwa kuwa wazi na bila ubadhilifu.

Rais wa Chama cha Madaktari ya Kikristo Tanzania,TCMA]Daktari Bwire Chilangi amesema hadi sasa kuna jumla ya Hospitali 102 na Hopitali teule 42 ,vituo vya Afya 106 na zahanati  zaidi ya 700 zilizochini ya Taasisi hiyo ya Kikristo hapa Tanzania ambazo zimekuwa zikishirikiana na Serikali ya katika kutoa huduma za afya kwa Watanzania.

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kadina Lugambo iliyochini ya Jimbo Kuu Katoriki  Dar Es Salaam katika Shirika la Mtakatifu Theresia Mtoto Yesu Sister Sarah Deogratius amesema amekuwa wakishrikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya mikataba ya utoaji wa huduma ya Afya.

Kuna zaidi ya Washiriki  400 wa chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania wamekutana Jijini Dodoma katika kujadili Masuala Mbalimbali ya Uboreshaji wa Huduma za Afya  wanatarajia kuhitimisha Sept.4.2019.