Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula, akizungumza na kikosikazi kinachoandaa kitini kwa ajili yakuwalimisha watoto kukabiliana na ukatili mitandaoni kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia NGO, Neema Lugangira
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku wakati akifafanua jambo wakati wa kikaokazi cha kudhibiti ukatili wa mitandaoni jijini Dodoma.
…………………………………..
KIKOSI kazi cha taifa cha kuzuia ukatili wa watoto mitandaoni wanajukumu la kuzuia kwa nguvu zote ukatili mitandaoni.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi maalumu (MCDGWSG), Zainabu Chaula leo Machi 31, 2022 wakati akizungumza na wanakikosi kazi hicho waliokutana jijini Dodoma kwa ajili ya kujengewa uwezo juu ya namna ya kuzuia na kuondoa maudhui ya Ukatili wa Mtoto Mtandaoni.
Amesema kuwa jukumu kubwa ni kukemea na kuelimisha jamii na isikie juu ya ukatili wa mtoto mtandaoni ambao unatweza utu wa mtoto.
“Ndugu zangu Uhalifu mtandaoni upo mhalifu hachagui nani wa kumdhalilisha mtandaoni.” amesema Zainabu.
Amesema Serikali imefanya juhudi ya kuunda kamati mbalimbali ikiwamo kamati ya kuzuia na kuondoa maudhui ya ukatili wa mtoto Mitandaoni.
Amewaomba wajumbe wa kikao kazi cha kuzuia na kuondoa maudhui ya Ukatili wa Watoto Mtandoni kuwa mabalozi wazuri na kuisambaza elimu hii isikike ili atakayekusudia kutuma maudhui ya ukatili kwa watoto mtandaoni ajisikie vibaya.
Zainabu amesema kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi maalumu (MCDGWSG) na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza afua katika kuhakikisha mtoto anakuwa salama dhidi ya ukatili ili kuhakikisha anakuwa na anafikia ukamilifu wake kwa maana akitukanwa naye anajisikia kutukana na akidhalilishwa nae anajisikia kudhalilisha.
Kikao kazi hicho kimehusisha wadau kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Katiba na Katiba, Wizara ya mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watekelezaji wa Sheria Ofisi ya Inspekta wa Polisi kitengo cha Makosa ya Mtandao, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP), Vyuo vya Elimu ya Juu, Mitandao ya Kijamii, wadau kutoka Vituo vya Redio na Televisheni na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala za Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Kikosikazi cha kudhibiti na kupambana na ukatili wanapitia na kuboresha mwongozo wa kupambana na ukatili wa mitandaoni, wakimsikiliza Katibu Mkuu ( Hayupo pichani) wakati wa kikao hicho. ( Picha zote na na Kitengo cha Mawasiliono Serikalini WMJJWM)
Baadhi ya wadau wa Kikosikazi cha kudhibiti na kupambana na ukatili wanapitia na kuboresha mwongozo wa kupambana na ukatili wa mitandaoni, wakimsikiliza Katibu Mkuu ( Hayupo pichani) wakati wa kikao hicho. ( Picha zote na na Kitengo cha Mawasiliono Serikalini WMJJWM)
Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira, akichangia mada wakati wa kikaokazi cha kudhibiti ukatili wa mitandaoni jijini Dodoma.
Inspekta Failuna Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku wakati akifafanua jambo wakati wa kikaokazi cha kudhibiti ukatili wa mitandaoni jijini Dodoma.
Zakia Msangi kutoka Shirika la WiLDAF akielezea jambo katika kikaokazi cha kudhibiti ukatili wa mitandaoni jijini Dodoma.
Picha ya Pamoja.