NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WATU watano wamefariki dunia pamoja na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya gari ya kampuni ya Dangote kugongana na gari nyingine kisha kuacha njia na kugonga nguzo ya umeme iliyosababisha shoti huko Kinayanya barabara kuu ya Kilwa -Kibiti.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Rufiji, Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo,usiku wa kuamkia agost 31.
Alieleza ,gari ya kampuni ya Dangote ikiendeshwa na dereva Feruzi Sukari akitokea Mkuranga kuelekea Kibiti aligonga gari T105 DGX T/premio ikiendeshwa na Yasin Njopeka (42) mkazi wa Kibiti akitokea Kinyanya kuelekea Kibiti na kuacha njia kisha kugonga nguzo ya umeme na kusababisha shoti ya umeme.
Lyanga alielezea ,watu hao watano kati yao wanne walikuwa katika gari la kampuni ya Dangote ambao ni Feruzi dereva wa gari hilo na wengine watatu ambao hawajatambulika baada ya kuteketea kwa moto,wakiwemo wanawake wawili na mwanaume mmoja.
Mwingine mmoja ni katika gari T105 DGX T/premio aitwae Siwema Said Kiumwa (39) mwalimu wa shule ya msingi Kinyanya.
Lyanga alimtaja majeruhi ni ,Yasin Njopeka mkazi wa Kibiti ambae ni dereva wa gari T 105 DGX.
Miili ya marehemu ilipelekwa hospital ya Mkuranga na baadae kwenda kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.
Majeruhi amelazwa katika hospital ya misheni Mchukwi kwa ajili ya matibabu.
Kamanda huyo alisema kwamba,chanzo cha ajali kinaendelea kuchunguzwa.
“Niwakumbushe madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali ,na wale watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria”alisisitiza.