Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Malikale Bw Wiliam Mwita akifungua kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
Picha ya pamoja ya wa Malikale, Makumbusho ya Taifa na Wajumbe wa kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar
…………………….
Na Sixmund J. Begashe
Makumbusho ya Taifa nchini imetakiwa kuimarisha mpango wa masoko ili uendane na mahitaji halisi ya wadau wa ndani na nje ya nchi ili kujenga uelewa na kuwawezesha kushiriki katika maendeleo ya kimakumbusho na Malikale
Hayo yamesemwa Mjini Bagamoyo na Bw Wiliam Mwita, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Mambo ya kale nchini, Dkt Kristowaja Ntandu alipofungua rasmi kikao kazi cha wadau wa Mpango wa Masoko wa Makumbusho ya Taifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa lengo la kuboresha mpango huo.
Licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa mkakati wa masoko, ameitaka Taasisi kuhakikisha mpango huo unaleta tija kwa jamii nchini ili iweze kuifahamu vyema Makumbusho ya Taifa na kunufaika nayo
Akiwasilisha Mpango huo kwa wadau wa kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga amesema kuwa Taasisi hiyo haijawahi kuwa na mpango wa Masoko hivyo, waliona ni muhimu kufanya hivyo ili kuisogeza Makumbusho kwa jamii.
Dkt Lwoga aliongeza kuwa, kazi ya kuandaa na kutekeleza Mpango wa Masoko ni moja ya majukumu ambayo yamepangwa kutekelezwa kwa lengo la kuongeza uelewa na kuvutia uwekezaji katika sekta ya makumbusho na malikale.
“Wataalamu wa mawasiliano wanaweka bayana kuwa ni vigumu kwa jamii kushiriki kikamilifu katika jambo la maendeleo endapo hawaelewi vizuri juu ya jambo husika, hivyo Mpango wa Masoko unalenga katika kuainisha mahitaji ya wadau ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuendeleza na kutangaza bidhaa za kimakumbusho na malikale” amesema Dkt Lwoga
Akizungumzia umuhimu wa Mpango wa Masoko kwa Taasisi, Dkt Patrokl Kanje ameshauri kuwa Maafisa Mahusiano kuwa karibu na vyombo vya habari hasa wahariri ili waweze kupata taarifa sahihi kuhusu Makumbusho ya Taifa na malikale kwa sababu wao wao ni sehemu muhimu sana katika jamiii.
Mwisho